Mkazi
wa Kijiji cha Bwekela wilayani Igunga mkoani Tabora, Kashinje Shima,
anatafutwa na Uongozi wa kijiji hicho, kwa kumpa ujauzito mwanawe wa
kumzaa mwenye umri wa miaka 17.
Ofisa
Mtendaji wa Kijiji cha Bwekela, ambaye pia ni Kaimu Ofisa Mtendaji wa
Kata ya Igoweko, Robert Ruhende, alilaani kitendo kilichofanywa na mzazi
wa mtoto huyo na kusisitiza kuwa sheria lazima ichukue mkondo wake.
Akisimulia
kisa hicho, mke wa mkazi huyo ambaye pia ndiye mama mzazi wa mtoto
huyo, Geni Njiro, alidai alibaini hali hiyo Julai 23 mwaka huu, baada ya
mwanawe wa kiume kumfumania baba yake na dada yake.
Kwa sasa kwa mujibu wa Geni, mwanawe huyo ambaye inadaiwa amekiri kushiriki kitendo hicho, ana ujauzito wa miezi saba.
Geni
alidai kabla ya kugundua kitendo hicho cha kinyama kilichokuwa
kikifanywa na mumewe, alihisi kuwa baba wa mtoto huyo alikuwa akitumia
mwanya wa yeye mama kutokuwepo nyumbani, kufanya vitu visivyo vya
kawaida.
Alidai
kuwa alipata hofu kuhusu mwenendo wa mumewe na mtoto wake siku moja
walipokuwa shambani wakiendelea na shughuli za kuvuna mazao, ambapo mumewe aliaga kurudi nyumbani.
Kutokana
na hofu hiyo, Geni alidai aliamua kumtuma mtoto wake mkubwa wa kiume,
ambaye hakutaka kumtaja jina, akafuatilie nyumbani kupata uhakika wa
kile alichokuwa akihofia.
Mama huyo alidai baada ya mtoto wake huyo kufika nyumbani, ndipo alikuta baba yake wakifanya ngono na mdogo wake na kurudi shambani na kumpa taarifa mama yake.
Baada
ya taarifa hiyo, mama huyo alidai kuwa aliamua kuita ndugu wa pande
zote mbili, kwa ajili ya kuzungumzia unyama huo, ambapo baba huyo
alipohojiwa katika kikao hicho cha familia, alikana kuhusika na tuhuma hizo.
Hata
hivyo, mama huyo alidai babu wa mtoto huyo, alishauri waende kupima
hospitali kupata ukweli, ndipo baba huyo alipokubali kuwa anatembea na
mtoto wake.
Baada
ya kukubali, inadaiwa baba huyo alitakiwa kulipa adhabu ya faini ya
ng’ombe wawili, ambao aliwalipa na suala hilo kuwa limekwisha.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mwina, Bundala Makelema, alikiri kuwepo kwa suala hilo.
Alidai
kuwa wakati mtuhumiwa huyo akilipa adhabu ya kimila ya ng’ombe wawili,
yeye alishiriki kwa nafasi yake ya Kiongozi wa Kitongoji.
Hata
hivyo, inadaiwa familia anayotoka mama huyo, ilipinga uamuzi huo wa
kifamilia na kumruhusu ndugu yao, kuchukua hatua zaidi, ikiwemo kutoa
taarifa katika vyombo vya habari.
Taarifa
hiyo ilipofika kwa Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Bwekela, ambaye pia ni
Kaimu Ofisa Mtendaji wa Kata ya Igoweko, Ruhende ambaye aliahidi kwenda
Polisi ili hatua zaidi zichukuliwe, mama huyo alidai ndipo mumewe
alipoamua kutoroka nyumbani na kwenda kusikojulikana.
No comments:
Post a Comment