Nini kinaendelea? Video Queen wa Bongo
anayeshikiliwa na jeshi la polisi nchini China kwa msala wa madai ya
kukamatwa na madawa ya kulevya ‘unga’, Jacqueline Fitizpatrick Cliff
‘Jack Patrick’ anadaiwa kuyeyuka gerezani.
Kwa mujibu wa ‘mtu wetu’ aliyeambatana na rafiki zake Jack kwenda
kumuona gerezani, Macau, Hong Kong nchini humo, walijikuta wakipigwa na
butwaa kuambiwa hakuna mtu kama huyo gerezani hapo hivyo kuibua hofu
kuwa huenda amenyongwa.
Uchunguzi wetu gerezani hapo ulibaini kwamba tofauti na hofu ya
rafiki zake, kuna uwezekano Jack amehamishiwa gereza lingine lililopo
nje kidogo ya Mji wa Macau.Chanzo chetu hicho kilidai kwamba habari za
ndani zilieleza kwamba Jack amehamishwa gereza hivyo kwa maelezo zaidi
watu wanaokwenda kumtembelea waende kwenye ofisi za gereza hilo
alilokuwa awali watapewa maelekezo wapi alipo mtu wao.
“Unajua watu wanaokwenda kumtembelea Jack gerezani ni Watanzania
walioko huku China kwa shughuli maalum hasa za sanaa, kama vile sarakasi
au maigizo, wengine wote wanaogopa, wanajua wanaweza kukamatwa.
“Tulipokwenda na mazagazaga yetu tuliambiwa Jack amehamishwa gereza
na inaonekana aliomba mwenyewe ila hatujui ni kwa nini alifanya hivyo,”
kilisema chanzo hicho.Hivi karibuni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Nje, John Haule alitoa taarifa na kutaja jumla ya watuhumiwa
waliokamatwa kwa kesi za madawa ya kulevya ambapo alisema kuwa kuna
Watanzania wengi wapo kwenye magereza mbalimbali China.
“Katika magereza ya China hadi Februari (mwaka huu) tulipewa taarifa
kwamba wapo Watanzania 177 magerezani na kati ya hao 15 wamehukumiwa
kunyongwa kutokana na baishara hiyo ya madawa ya kulevya,” ilisema
taarifa hiyo ya katibu mkuu.
Jack alikamatwa Macau, Hong Kong, mwaka jana hivyo kesi yake
inaendelea kuunguruma. Tofauti na Beijing ambao huwa wananyonga watu
wanaojishughulisha na unga, Hong Kong ni kifungo cha miaka kadhaa tu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment