Usipomuona mpenzi wako kwa muda moyo huingia upweke, matamanio ya
kumtaka kumuona huongezeka mara dufu, mawazo ya jinsi alivyo na kila
kitu kuhusu yeye hukufanya utabasamu na kufurahia uwepo wake kila
umuonapo, na hukupa hisia na tamaa ya kutaka kumuona zaidi na kukufanya
hitajio la kuwa naye kukuwa na hamasa zako juu yake kuongezeka na
kumpenda zaidi.
Vivyo hivyo iwapo muda mrefu ukipita bila kumuona mpenzi wako upweke
huzidi na moyo huchoka, hamasa na taamaa zinabadilika kuwa mzigo, mawazo
mazuri ya kimapenzi na husuda hubadilika kuwa msongo, njisi muda
unavyozidi kwenda na ndivyo hamasa ya mpenzi wako ndivyo inavyoisha na
kuzidi kushuka, moyo unasahau mguso wake aliokuwa nao kwako, shauku ya
kuongea inapungua, kama mlikua mnaongea kila baada ya masaa mawili
kwenye simu, masaa yatabadilika na kuwa matatu, yakiwa matatu
yatabadilika kuwa siku nzima, umbali unakuwa tena hautengenezi upweke wa
kutaka kuonana bali unawafanya mioyo yenu kusahauliana na umbali wa
hisia kati yenu kuongezeka.
Waulize wanaume imekuandalia njia tano za kuongeza hamasa na kuondokana
na upweke unaosababisha hisia kupungua pamoja na mvunjiko wa mapenzi
ndani ya mahusiano ya mapenzi ya umbali, ukitaka mambo yako yaende
salama hakikisha unazingatia njia hizi muhimu.
- Namba 1, Hakikisha unaongea kile kilicho moyoni mwako.
Wanawake
wanauwezo mkubwa wa kugundua iwapo kuna kitu kinakusumbua na vile vile
wanawake ni rahisi sana kujihisi, kama wamekugundua umeudhika na
usipokielezea mapema akiwa amekuuliza, moja kwa moja ataanza kujifikilia
ni yeye ndio aliyesababisha au ni kwa ajiri ya uhusiano kwa sababu yuko
mbali unakuwia vigumu ila unakuwa hautaki kuelezea wazi, kwahio kwa
mahusiano ya mbali inakubidi uwe mwangalifu na mvumilivu, kama kuna kitu
kati yenu hakiendi vizuri, ni vizuri mkakiongea kwa wakati ulio
mwafaka, iwapo mkakiacha kikawajengea kinyongo ndani ya mapenzi yenu na
kufikia hatua ya kuudhiana, ugonvi wa mapenzi kwa wapenzi walio mbali ni
mgumu sana kusuruhishwa.
- Namba 2, Hakikisha mnapanga jinsi ya kukutana.
Umuhimu
wa kukutana na kuonana ana kwa ana ni mkubwa sana hasa kwa mapenzi ya
mbali, kukutana huamsha hisia na mvuto ndani ya mapenzi uliosahaulika, muda
ni dawa ya kusahau kwahio iwapo mkiacha kukutana kwa muda mrefu, yale
maumivu yanaosababishwa na upweke wa kutomuona mpenzi wako huisha na
hamasa za mapenzi pia hupungua, binadamu ameumbwa kubadilika kutokana na
mazingira, kwahio mkiruhusu muda mrefu kupita bila kuonana utofauti
lazima utaingia kati yenu hata kama mlikua na mapendo makubwa kiasi
gani, umuhimu wa kuongea hautokuwepo tena na hisia zitapolomoka na
kusababisha mvuto kuisha kabisa ndani ya uhusiano wenu.
- Namba 3, Fanyeni vitu kwa pamoja mkiwa mbali.
Kwa
tekenolojia ilivyongezeka kipindi hichi, hamuhitaji muwe mji au mtaa
mmoja ili muweze kufanya kitu cha kuwafurahisha pamoja, tafuteni kitu
kipya cha kuongelea iwe filamu au kitu chochote kingine ambacho wote
wawili mnafurahia na kupenda kukifanya au kufuatilia, mnaweza pigiana
simu na kutaalisha filamu na wote mkaanza kuiangalia kwa wakati mmoja,
pande zote mbili mnatakiwa kuwa wabunifu na mapenzi hayatawezekanika
iwapo upande mmoja pekee ukiwa unajitahidi wakati mwingine unategea na
kutokujali, na kila mkiongea hakikisha hamtumii sana neno nimekumisi,
chochote kikiwa kinatamkwa sana na kusikiwa kila siku hupoteza mvuto na
kuwa neno la kawaida na kusababisha maongezi kuisha mapema.
- Namba 4, Tambulishaneni kwa marafiki wapya na usiwe na wivu na marafiki wake wa kiume.
Kitu
kimoja uhusiano wa mbali unachosababisha ni kutoa muda mwingi wa
kutumia na marafiki, kazi yako kama mpenzi wake unatakiwa usionyeshe
wivu wako maana utakuona humuamini na kusababisha asikushilikishe kwenye
baadhi ya mambo mengine maana anajua iwapo akifanya hivyo hautohafiki
na zaidi ya hapo itasababisha ugomvi ambao haupo na itamfanya pia na
yeye kuwa na wasi wasi na wewe pia, kujiamini na kutomtilia mashaka
mpenzi wako kunatengeneza hali ya kuaminiana na kusababisha uhusiano
ujijenge katika hali nzuri ya amani na yenye msimamo zaidi.
Kutambulishana kwa marafiki wapya inawafanya muwe huru na kupata mengi ya kuongea.
- Namba 5, Ongeeni kwa kutumia njia za kuonana mara kwa mara.
Tumieni
tekenelojia iliyopo kuongeza hamasa, mvuto na chachu ndani ya mapenzi
yenu, kuonana ana kwa ana kwa kutumia njia za skype, google talk au
kutumiana video kwenye whatsaap kunaleta hali ya uhalisia zaidi na
kufanya kusimuliana kuhusu kitu cha kijinga rafiki yako alichokifanya au
mfanyakazi mwenzio anavyokuboa kuwe na hali ya mawasiliano yenye mvuto
zaidi.
Kuona
tena tabasamu lake na jinsi uso wake unapotabasamu kulipua hisia zako
maradufu na za kwake pia na kusababisha hamasa na hisia zilizosahaulika
kurejea tena kwa mara nyingine.
No comments:
Post a Comment