Tumezoea kuona kwenye filamu au tamthilia simulizi la msichana mrembo anaotoka katika familia ya kitajiri aliyechagua kuyaacha maisha ya raha na kuishi uswahilini na kijana anaempenda.
Huko
Kenya, kumeripotiwa tukio halisi lililovuta hisia za wengi na
kuzungumzwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari,
ambapo msichana wa kihindi ameamua kuachana na familia yake tajiri na
kuambatana na kijana wa Kenya aliyezama nae kwenye vilindi vya mahaba.
Msichana
huyo wa kihidi anayefahamika kwa jina la Sarika Patel, ameolewa na
kijana wa kabila la Bukusu, Timothy Khamala uamuzi ambao ni nadra
kutokana na mila na desturi za kihindi na kilichoshangaza zaidi ni kuwa
wawili hao wanaishi maisha duni kijijini.
Kwa Sarika, maisha ya umasikini sio kikwazo cha kulipata penzi la kijana Timothy aliyenasa kwenye penzi lake.
Safari
ya penzi la Sarika na Timothy ilianzia nyumbani kwao Sarika ambapo
kijana Timothy alikuwa akifanya kazi na baadae kutimuliwa kwa kudhaniwa
kuwa ana uhusiano na princess wa jengo hilo (Sarika) jambo ambalo
lilikuwa kweli.
Wawili
hao wamejitoa na kuendelea kuishi pamoja licha ya kukiri kuwa
wanakabiriwa na changamoto kubwa ya kutengwa na jamii ya upande wa
familia ya kwao Sarika kwa kuwa kitendo hicho sio sahihi hata kidogo kwa
mujibu wa mila na desturi zao, ambapo watu wa jamii sawa ndio
wanaooana.
Hata
hivyo, Sarika ameelezea msimamo wake kuwa utofauti wa rangi na tamaduni
au ufukara wake hauwezi kumtenga na mpenzi wake wa dhati Timothy.
Mapenzi sio pesa, mapenzi ni moyo
No comments:
Post a Comment