skip to main |
skip to sidebar
MWALIMU MKUU AFUNGUA BAA NDANI YA ENEO LA SHULE
Baada
ya siku chache kugundulika kuwa Mwl.Mkuu wa shule ya Msingi Unenamwa
kata ya Luwumbu wilayani Makete Mkoani njombe anauza pombe za kienyeji
na viwandani kwenye nyumba ya shule hiyo hali hiyo imethibitishwa leo na
wananchi wa kijiji hicho
Wakizungumza katika mkutano uliofanywa na Mratibu wa Elimu kata ya
Luwumbu Bw.Burton Mbedule wamesema kuwa ni kweli Mwl.Mkuu wa shule ya
Msingi Unenamwa Evaristo Maginga amefungua kisiri kilabu cha kuuza Pombe
za kienyeji na viwandani katika nyumba ya shule hiyo
Katika Mkutano huo mratibu elimu kata Bw.Mbedule aliwataka wananchi wa
kijiji hicho kumthibitishia taarifa hizo kama ni kweli kwani amesema
yeye aliposikia taarifa hiyo alimuona Mwenyekiti na kuzungumza naye
kuhusu uvumi huo,baada ya hapo alikutana na mwalimu huyo ambapo
alimwambia mratibu huyo kuwa anataka anataka uthibitisho wa watu
waliokuwa wanapata huduma hiyo kwake
Baada ya hapo amesema aliwatafuta wananchi kabla ya kuitisha Mkutano
huo ambapo wananchi walimweleza kuwa taarifa za mwl.huyo kutengeneza
pombe ni kweli na si kuuza pombe eneo la shule
Bw.Mbedule Alipowataka wananchi kumthibitishia taarifa hizo katika
Mkutano huo uliokuwa chini ya Mwenyekiti wa kijiji Bw.Labson Tweve
wananchi wamesema kuwa huwa wanajipatia huduma hiyo katika nyumba hiyo
hata kwa Oda na sio uongo kwamba huduma hiyo haipo shuleni hapo kwani
wamekuwa wakiipata nyumbani hapo
Akizungumza
na Kitulo fm Mwl. huyo siku ya Alhamisi wiki iliyopita katika kipindi
cha Morning power alikana taarifa hizo na kusema kuwa kuwa yeye anauza
vitu vidogovidogo na si Pombe
Hata hivyo wazazi wa watoto wanaosoma katika shule ya Msingi Unenamwa
wameeleza kukerwa na elimu duni itolewayo na walimu waliopo shuleni hapo
kwani wamekuwa wakikagua madaftari ya watoto wao na kusema ni tofauti
na wanafunzi wanaosoma katika shule jirani kama Idende
Hivyo baadhi yao wamelazimika kuwahamisha watoto wao katika shule hiyo
na kuwapeleka shule nyingine ya Idende kwa kuhofia watoto wao kupata
elimu Duni kwani endapo wakipelekwa Sekondari watakuwa na Uelewa Mdogo
Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamesema hawajapendezwa na tabia ya
walimu wa shule hiyo kwani wanafunzi wamekuwa wakifanya vibarua muda wa
masomo kutoka Unenamwa hadi Mwakavuta kitu ambacho kinaongeza kufeli kwa
wanafunzi kitaaluma
Hatma ya Mkutano huo wananchi wamemtaka Mratibu Elimu wa kata hiyo
kuzungumza na Mwl.huyo na kumuonya mara moja aache biashara hiyo katika
eneo la shule
No comments:
Post a Comment