Binadamu
wanayo mabadiliko ya kiasili, hasa tunapozungumzia matendo yao,
uaminifu na majaribu. Ni wadanganyifu na hupenda kuficha tabia zao nyuma
ya sababu za uongo na kweli. Wakati
wanawake hulaumu kwamba vitendo vya wanaume havitabiriki, lakini bado
upo ukweli kuwa jinsia ya kike hujiona sahihi. Wao hudhani wanatabirika.
Hata hivyo, unachotakiwa kuaamini ni hiki, A na B yote ni sawa.
Wanaume
wanatabirika na wanawake ni kinyume chake. Asili ya wanaume ni kuwa
wanapotoka, hukumbuka nyumbani. Kawaida yao ni kama msemo: “Mwenda tezi
na omo marejeo ngamani.” Mwanaume
akipata kitu ‘comfotabo’ cha pembeni ni nadra kumsahau ‘mamsapu’
nyumnbani. Hawadharau dafu, wanaamini embe ni tunda la msimu. Kinyume
chake ni kuwa mwanamke akionjeshwa ‘asali ya nje’ huchonga mzinga.Tunakaa
meza moja na watu mbalimbali wenye matatizo kwenye uhusiano.
Tunawashauri nini cha kuzingatia, wanayafanyia kazi yale ambayo tunawapa
na kunyookewa. Hilo linakuja na tafsiri kwamba tunawajua watu wengi na
kasoro zao kimapenzi.Udhaifu
mkubwa wa wanawake ni huu, hawajui kutofautisha maziwa na tui la nazi.
Wanahadaika kwa weupe na kudhani A na B ni sawa. Hiyo ndiyo sababu ya
kumuona ‘mista’ wake hafai na kujisajili kwa ‘Kiserengeti boy’.Ni
rahisi kumbaini kama ameanza kuchepuka kwenye njia za panya, kwani
akipewa tamu nje, hurudi nyumbani na gunia la dharau na matusi kwa mume
wake. Akiombwa unyumba kila siku atatoa visingizio.Ataanza
kumzingatia zaidi yule anayemtosheleza katika matamanio ya mwili na
mume wake atampa ‘kadi nyekundu’. Ikiwa mzee ndani maisha yake ni pangu
pakavu tia mchuzi, kisha apate kibopa anayeweza kumpa pesa ya ‘shopping’
Sabasaba, ujue wa zamani lazima atapewa kibuti. Kinyume
chake ni kuwa hauwezi kusikia mwanaume anamuacha mpenzi wake kwa sababu
hawezi kutoa mahanjumati kitandani au maisha ni magumu.Hata
hivyo, lengo kuu ni kutaka kujua alama za hatari kwa mpenzi wako, yaani
ukizisoma kwake, basi utatakiwa ujiandae kupewa ‘red card’.
MUDA WOTE YUKO MBALI
Ukimuomba
‘appointment’ haishiwi sababu, mara oh! Nyumbani kuna hili na lile au
anakuahidi atakuja lakini mwisho wa siku hatimizi ahadi. Anasingizia ana
kazi nyingi kusudi asionane na wewe. Hiyo ni alama ya hatari, ujue siku
si nyingi atakuacha solemba. Wengine
wameumbwa na aibu, kumtamkia mtu sikutaki ni kazi kubwa, hivyo huamua
kujiweka mbali ili ujiulize mwenyewe kichwani na kupata jibu kuwa tayari
ndege amekwisha choropoka tunduni.Kama
ni mume, ugomvi kidogo anaondoka na harudi mpaka kesho yake, au mke
ndani ukimtibua anafungasha virago vyake na kurudi kwao ama kuweka
hifadhi kwa marafiki zake, hiyo ni ishara kuwa hataki kuwa karibu na
wewe, hivyo hakutaki.
HATAKI KUFANYA MAPENZI
Kila
mtu hufurahia mapenzi na yule anayempenda kutoka moyoni, labda awe
amechoka. Lakini inapotokea mara kwa mara kila unapoomba anakupa sababu
tofauti za kukutolea nje, hiyo ni alama kuwa amekuchoka.Mapenzi
ni tendo la moyoni, linalotambaa mwilini kwa hisia, hivyo lipo
kisaikolojia zaidi. Pointi hiyo ndiyo inayotoa ukweli kuwa kama hataki
kufanya mapenzi na wewe, maana yake moyoni mwake haumo.
ANAKUWA MPINZANI
Wakati
mnatongozana alikuwa anakusifia kwa kila kitu. Ulipovaa alikuambia
umependeza, alikupongeza kuwa sura na umbo lako ni ‘matata ile mbaya’.
Mlipokutana kwenye sekta ‘chumbani zaidi’, huko pia alikumwagia sifa
kemkemu.Tofauti
na wakati huo, hivi sasa kila unachokifanya kinakuwa ni kibaya kwake,
ukimpigia simu anakuambia umpe nafasi ya kufanya kazi, yupo ‘bize’.
Ukivaa, anasema mavazi yako hayafai kuongozana naye.Hata
siku moja, mpenzi hawezi kuwa mpinzani, kama kuna mambo hayaendi sawa,
basi atapigana kukubadilisha ili uende sawa na yeye, lakini kama
anakuponda bila kukupa ushauri, hiyo ni alama ya hatari kwako. Mkiwa
katika maongezi yenu wawili au yanayojumuisha baadhi ya marafiki,
hataki kuwa upande wako. Anaweza kumsifia mtu mwingine kuwa ni mzuri
kuliko wewe, hilo unatakiwa kulisoma na kushika njia mapema.
ANAANZISHA UHUSIANO NA MTU MWINGINE
Akufukuzae
hakwambii toka, vitendo vyake vitakuonesha tu! Hivi kama mtu anakupenda
kwa dhati, anawezaje kuanzisha uhusiano na mtu mwingine? Jibu
ni kwamba hawezi, kwahiyo ni busara uwe unasoma alama za nyakati ili
maji yanapofika shingoni uwe umeshapata njia ya kukutoa kimasomaso.
ANASEMA HATAKI KUKUONA
Baada
ya kukufanyia vituko vya kila aina, sasa ameamua kukuweka wazi kuwa
hataki kukuona kabisa, sasa unangoja nini kwake? Hautakiwi kuwa mtumwa
wa mapenzi, mpende akupendaye, asiyekupenda achana naye.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment