Mashabiki wakimng'ang'ania msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ wakati wa shoo ya nani kama Mama.
Katika usiku huo, wiki iliyopita, Ommy Dimpoz alikuwa akimsindikiza
Christian Bella, aliyekuwa akizindua albamu yake iitwayo Nani kama Mama.
Ommy Dimpoz alifanya makamuzi ya nguvu ambapo warembo kadhaa walimvaa
jukwaani na kumng’ang’ania, huku wakionekana kuzungumza maneno ya
kumshawishi kimahaba, lakini mkali huyo wa kibao cha Baadaye
‘aliwapotezea’.
No comments:
Post a Comment