HISIA! Mrembo aliyetinga hatua ya Tano Bora ya
Shindano la Bongo Star Search (EBSS) 2013, Maina Thadei ameibuka na
kuelezea hisia zake kuwa anateswa na penzi la staa wa Bongo Fleva,
Asilahi Isihaka ‘Aslay’.
Akizungumza na gazeti hili, Maina alisema kuwa ameshindwa kabisa
kuzizuia hisia zake kwa bwa’mdogo huyo ambaye anatamba na wimbo wa Ya
Moto na kusema yupo tayari kwa lolote.
“Kwa kweli ananinyima usingizi, namfikiria sana. Naanza kazi moja tu
ya kumsaka na nikimkamata hatoki hapa kwangu, sitakubali,” alisema
Maina.
Pia mwanamuziki huyo aliongeza kuwa, atakapokuwa karibu na Aslay
anaamini watatengeneza ‘kapo’ nzuri ambayo italeta ladha pindi
watakaposhirikiana kimuziki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment