Sakata la madai kuwa mke wa aliyekuwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, Stella Barlow
(pichani)alitimuliwa ukweni kwa mapanga limechukua sura mpya baada ya
ndugu wa mumewe kuibuka na kutoa ufafanuzi.
Mjane Stell Barlow wakati wa mazishi ya aliyekuwa mume wake, Kamanda Liberatus Barlow.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu mwishoni mwa wiki
iliyopita, ndugu wa marehemu Kamanda Barlow, aliyejitambulisha kwa jina
moja la Lyimo alisema si kweli hata kidogo kuwa walimkimbiza kwa mapanga
shemeji yao huyo.
“Kilichotokea ni kwamba tulimuambia huyo
mama kuwa hawezi kufanya chochote kwenye kaburi la mumewe mpaka akamuone
kiongozi wa ukoo. Kimila tangu wakati kaburi linachimbwa, linakuwa
chini ya uangalizi wa wanaume na hata baada ya kuzika haliwezi kuwa
chini ya mwanamke, hilo tulimjulisha,” alisema Lyimo.
Alifafanua kuwa wamewahi kufanya misa ya kumuombea marehemu Barlow na
ndugu wengine na mama huyo aliarifiwa lakini hakuja. “Ujumbe wetu ni
kwamba muambieni huyo mama kuwa siyo vizuri kuchafua ukoo kwa sababu
hatuna ugomvi naye na hakika kama ni wa kulaumiwa ni yeye siyo sisi wana
ukoo,” alisema Lyimo.Wakati huo huo, kwenye Gazeti la Uwazi la Agosti 27 mwaka huu tuliweka kimakosa picha ya mke wa marehemu Kamanda James Kombe badala ya mke wa kamanda marehemu Liberatus Barlow, Stella Barlow. Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliowapata wahusika- Mhariri.
No comments:
Post a Comment