Shahidi
wa kwanza katika kesi ya kubaka inayomkabili mwimbaji wa nyimbo za
Injili, Emmanuel Mbasha, ameieleza mahakama jinsi mshtakiwa alivyomkaba
shingo na kumziba mdomo kwa kutumia nguo, kisha kumbaka.
Shahidi
huyo ambaye ni shemeji yake, mwenye umri wa miaka 17, aliyasema hayo
jana wakati akitoa ushahidi wake katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala.
Hata
hivyo, kesi hiyo ilisikilizwa kwa faragha(Chamber Cort) baada ya
Mwendesha Mashtaka wa Serikali Nassoro Katuga kuiomba mahakama kesi hiyo
kuendeshwa kwa faragha kwa kuwa imefikia hatua ya kusikilizwa na sheria
inaonyesha kuwa mtoto huyo yupo chini ya miaka 18.
Ombi
hilo lilikubaliwa na pande zote mbili na kesi hiyo kuendeshwa katika
mahakama ya faragha na Hakimu, Wilbaforce Luhwago aliomba watu wote
walikuwepo ndani ya mahakama hiyo kutoka nje ili kupisha upande wa
mashtaka kutoa ushahidi.
Akiongozwa
na mwendesha Mashtaka wa Serikali Nassoro Katuga, shahidi huyo alidai
siku ya tukio, Mei 23, mwaka huu, mshtakiwa aliondoka na mke wake kwenda
kufuatilia mkanda wa video lakini ghafla alirudi nyumbani kwake Tabata
Kimanga akiwa peke yake.
Alidai
siku hiyo ya tukio mshtakiwa alifanikiwa kufanya mapenzi na binti huyo
na kumwambia asimwambie mtu wakati mke wake akiwa hayupo nyumbani hapo.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 12,2014.
No comments:
Post a Comment