Mshindi
wa Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 Mwanaafa Mwinzago (Katikati)
akisindikizwa na Matron pamoja na Mfanyakazi wa TMT huku akilindwa na
Mabaunsa wakati alipopelekwa Katika Mitaa ya Kariakoo kwaajili ya
kununua zawadi Kwaajili ya Wazazi wake.
Mfanyakazi
wa TMT, Happy Ngatunga (Kushoto) akitoa maelekezo kwa Mabaunsa na
Mshindi wa TMT aliyejinyakulia Kitita Cha Shilingi milioni 50 katika
fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 iliyofanyika mwishoni mwa
wiki katika Ukumbi wa Mlimani City Mwanaafa Mwinzago wakati walipokuwa
katika matembezi Kariakoo.
Baadhi
ya wafanyabiashara wa Kariakoo wakimpungia Mikono kama ishara ya
kumpongeza kwa kuibuka mshindi wa fainali ya Tanzania Movie Talents
(TMT) Star wa TMT 2014 kutoka Mtwara, Mwanaafa Mwinzago Wakati
alipokatiza kwenye mitaa ya Kariakoo pindi alipokwenda kununua zawadi
kwaajili ya wazazi wake
Star
Wa TMT 2014, Mwanaafa Mwinzago (katikati) akiwa na furaha mara baada ya
kupongezwa na mashabiki waliopata nafasi ya Kumsalimia na kumpongeza
wakati akikatiza mitaa ya Kariakoo pindi alipokwenda kununua Zawadi
kwaajili ya Wazazi wake
Wanafunzi
wa Shule ya Msingi wakimpongeza Star Wa TMT 2014, Mwanaafa Mwinzago kwa
kuweza kuibuka mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014
kwa kuwabwaga mwenzake 9 na kuondoka na Kitita Cha Shilingi Milioni 50
za kitanzania wakati walipomuona katika moja ya mitaa ya Kariakoo wakati
Star Huyo wa TMT 2014 alipokwenda Kununua Zawadi kwaajili ya kuwapatia
wazazi wake ikiwa kama ishara ya Upendo na shukrani kwao.
Matron
wa Kambi ya TMT 2014, Kemmy akichagua baadhi ya vitenge kwa Niaba ya
Star Wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago wakati alipopelekwa Kariakoo kwaajili
ya Kununua Vitenge kama zawadi kwa wazazi wake.
No comments:
Post a Comment