Hatimaye
Spika wa Bunge la Tanzania pale Dodoma atakuwa na makazi rasmi baada ya
ujenzi wa nyumba ya Spika kukamilika na makabidhiano kufanyika. Nyumba
hiyo ambayo ipo maeneo ya
Uzunguni
nje kidogo ya Dodoma mjini imegharimu takribani Tshs 1.5 Billion na
imejengwa na kampuni ya Pacha Building Construction Company. Hii inakuwa
nyumba ya kwanza rasmi ya Spika kwani hapo awali hapakuwahi kuwa na
nyumba rasmi ya Spika.
No comments:
Post a Comment