Taharuki hiyo ilikuja pale Nisha alipoegesha gari lake eneo hilo na kushuka kisha wanafunzi na watu wengine kusitisha shughuli na kumzunguka kutaka kujua kulikoni staa huyo kufika eneo hilo linaloaminika kuwa kila anayekwenda ni muumini wa imani ya Freemason.
Baadhi ya watu walimuuliza Nisha alichofuata kwenye hekalu hilo huku mwenyewe akishindwa kujibu kwani alitupiwa maswali mfululizo.
Chanzo chetu kilidai kuwa msanii huyo baada ya kuona amezingirwa na watu alisimama na kuzungumza nao kisha akabadili uamuzi, alirudi ndani ya gari na kuondoka eneo hilo ambapo baadhi ya watu walidai huenda alitaka kuingia kwenye hekalu hilo kama mastaa wenzake ambao mara nyingi huonekana wakiingia na kutoka.
Upande wa mbele wa Hekalu la Freemason lililopo karibu na hoteli ya Hyatt Regency Posta, Dar es Salaam.
Kufuatia taarifa za chanzo hicho, gazeti hili lilimsaka msanii huyo
na kufanikiwa kumpata kwa njia ya simu ambapo alifafanua kuhusu suala
hilo."Aah! Dah, nyie habari hizo mmezipataje, mbona pale sijaona
mwandishi yeyote? Ukweli pale mimi nilipaki gari tu kwa ajili ya kufanya
mambo yangu maeneo yale lakini ghafla nikashangaa umati umenivaa, kila
mtu anataka kuniona laivu na kuongea na mimi.“Wanafunzi ndiyo usiseme, sasa kutokanana na kusongwa na umati kama ule nikabadili maamuzi na kuondoka zangu,” alisema Nisha.
Kumekuwa na dhana miongoni mwa watu kwamba, baadhi ya mastaa wenye mafanikio Bongo wamejiunga na imani ya Freemason huku ikisemekana wanaishi kwa kuabudu kwenye hekalu hilo mara moja kwa wiki.
Hata hivyo, hakuna ushahidi wa moja kwa moja ni staa gani mwanachana wa Freemason kwani hakuna aliyewahi kukiri kwamba yeye ndiye.
No comments:
Post a Comment