Sehemu ya majeraha aliyoyapata Magdalena Elisha baada ya kusulubiwa na mama huyo. HII ni too much! Jalada namba KW/RB/7565/2014-SHAMBULIO LA
KUDHURU MWILI lililopo kwenye Kituo cha Polisi cha Kawe, Dar, linamhusu
mama aliyetajwa kwa jina moja la Teddy, mkazi wa Tegeta kwa madai ya
kumtumikisha na kumtesa mtoto Magdalena Elisha (10) na kumsababishia
majeraha na makovu ya vidonda sehemu mbalimbali mwilini.
Habari kutoka ndani ya jeshi la polisi zilidai kwamba, Teddy
alimchukuwa mtoto huyo jijini Arusha kwa lengo la kumsaidia kukaa na
mwanaye kwa kuwa familia ya mtoto huyo haina uwezo na ameishia darasa la
tatu kwa kukosa vifaa vya shule.
Kwa mujibu wa Teddy, bila kujua kwamba ni kosa kumwajiri mtoto,
aliamua kumwadhibu mtoto huyo kutokana na kutomsikiliza bosi wake hasa
alipokuwa akionywa kuachana na tabia ambayo haikuwa ikimfurahisha.
Kwa upande wake Magdalena alidai kwamba alikuwa akipokea kipigo kila
siku hasa wakati mama huyo alipokuwa akirejea nyumbani kutoka ‘jobu’ na
kukuta mwanaye analia.
“Alikuwa akinipiga kila siku akikuta mtoto (wa miaka miwili) analia.
Pia kuna siku alinipiga sana asubuhi, nikaona nikimbilie kwa mjumbe,
ndiyo tukaenda kituo cha polisi, tukakutana naye akiwa anatoka polisi
kutoa taarifa kuwa nimepotea, mimi naomba nisaidiwe nirudi kwa mama
yangu Arusha,” alisema Magdalena na kumfanya bosi wake huyo apewe kibako
na vyombo vya sheria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment