BREAKING NEWzz: MSANII 'M2 THE P' ALIYEPELEKWA HOSPITALI PAMOJA NA MANGWAIR NAYE AFARIKI DUNIA, NI MSIBA JUU YA MSIBA...!!

Pichani ni marehemu Albert Mangwair akiwa na M2 the P.  

Taarifa zilizothibitishwa kutoka nchini Afrika Kusini ni kwamba yule msanii aliyepelekwa hospitali pamoja na Mwana Hip Hop, Albert Mangwair aitwaye M to the P naye amefariki dunia leo.


 M2 the P alipelekwa katika hospitali ya St Hellen iliyopo jijini nchini humo kwa matibabu baada ya kukutwa amepoteza fahamu akiwa na Mangwair aliyefariki dunia jana. 

Miili ya marehemu hao bado ipo katika hospitali ya St. Hellen na mipango ya kuhamisha miili hiyo bado inaendelea hivi sasa.
 
Taarifa zisizo rasmi zinadai kuwa yawezekana Mangwair na M2 the P walikula chakula chenye sumu ambacho kimepelekea mauti hayo.

 Baadhi ya Watanzania waishio nchini Afrika Kusini wamejikusanya kwa ajili ya kuandaa mipango ya kuhifadhi miili hiyo pamoja na safari

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger