LATEST NEWzz: MSANII 'M2 THE P' ALIYEPELEKWA HOSPITALI PAMOJA NA MANGWAIR NAYE YUPO HOI HOSPITALINI...!!

Taarifa zilizotufikia ni kwamba msanii Albert Mangwair asubuhi ya leo alipelekwa hospitali pamoja na msanii M2 the P ambaye kwa sasa yupo hoi katika hospitali ya St Hellen Afrika Kusini. Mangwair amepoteza maisha leo saa 9 alasiri baada ya kupelekwa hospitalini hapo akiwa hajitambui. Kwa mujibu wa Hussein Original aliyeko jijini Pretoria nchini Afrika Kusini ni kwamba Mangwair alikuwa anakaa gheto moja na msanii M2 the P na asubuhi ya leo walienda kuwagongea na kuwakuta wote wamezima katika chumba chao. Mangwair na M2 the P walitakiwa kurudi jijini Dar es Salaam leo. Mungu ailaze roho ya Mangwair mahali pema peponi.


Mangwair akiwa katika pozi na msanii M2 the P
 

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger