BAADA ya mwanamuziki Baby Joseph Madaha kunaswa na mtego wa
kujiuza uliotegwa na gazeti hili hivi karibuni, mdada huyo anaonekana
kubadilika na anadai mgogoro uliojitokeza kati yake na meneja wake, Joe Kairuki
kutokana na tukio hilo umekwisha.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni msanii huyo ambaye ni kati
ya wasanii wa kike wanaofanya vizuri alisema, tukio lile limefanya ajifunze
kitu na kubadilika kwake kumesababisha bosi wake amsamehe na waendelee kupiga
mzigo.
“Kweli nimejifunza kutokana na makosa maana kunaswa
kwenye ule mtego kumenigharimu sana lakini nashukuru nimesamehewa na mkataba
ninaendelea nao, yale yamepita na sasa ni kazi tu,” alisema Baby Madaha a.k.a
The Queen of Swaga.


No comments:
Post a Comment