Showing posts with label BABY MADAHA. Show all posts
Showing posts with label BABY MADAHA. Show all posts

BABY MADAHA ANUSURIKA KUBAKWA TENA, MASHABIKI WAMTIA VIDOLE KWENYE UTAMU

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhTbOG479tSQAwbMuZfmWOa2dwNZAQ-uFiCWDd6EpQs3ViZHsExgB1X_I0UMqnQ8HwwyggCeIQbPfjbDVQW5xADwU4hBpbonziR5rOzNQ_FZ77lLMp2KSMYKSycbFnYuor5SRKTmR3hL6Jh/s640/Image536.jpgMsanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Baby Joseph Madaha amenusurika kubakwa nchini Kenya baada ya kupanda jukwaani akiwa ametinga kivazi cha nusu utupu.
Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita katika mji wa Naivasha uliopo Nairobi nchini humo ambapo mwanadada huyo alipopanda jukwaani akiwa amevaa sketi fupi iliyokuwa imeacha sehemu....
Read more >>

BABY MADAHA AMWAGANA NA MENEJA WAKE, SOMA ZAIDI HAPA

STAA wa filamu Bongo, Baby Joseph Madaha amemwagana na aliyekuwa mwandani wake ambaye pia ni meneja wake, Joe Kairuki pasipokuwa na sababu za wazi.
Staa wa filamu Bongo, Baby Joseph Madaha akiwa na Meneja wake, Joe Kairuki.
Chanzo chetu cha kuaminika kilichoomba hifadhi ya jina lake kimetutonya kuwa, Madaha na Joe wamebaki kuwa mtu na bosi wake ila msanii huyo sasa amejiweka kwa mwanaume mwingine.
Katika kujua ukweli wa ishu hiyo, mwandishi wetu alimpigia simu Madaha ambaye alisema: “Hee unaniuliza kuhusu Joe, mbona umechelewa kujua? Nimeachana naye, sasa nimejipatia mpenzi wangu mwingine na tunapendana kupita maelezo.”
Read more >>

SHILOLE NA BABY MADAHA WAANZISHIANA BIFU ZITO, CHEKI ZAIDI HAPA

MTIFUANO mzito umeibuka kati ya mastaa wa Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na Baby Madaha baada ya kurushiana vijembe.
Staa wa Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Awali katika gazeti la Amani toleo la wiki iliyopita, Baby Madaha alinukuliwa akisema kuwa Mwezi wa Ramadhani unambana kiuchumi, kwa vile kumbi nyingi za starehe zimefungwa, hivyo anakosa shoo.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Shilole alisema anamshangaa Madaha kwa kukosa hofu ya Mungu, huku akimchana kuwa, haweki akiba, anaishi maisha ya kutegemea shoo ndiyo maana anaulalamikia mwezi huu.
Baby Madaha.
Madaha alivyoelezwa kuhusu maoni ya Shilole, alikuja juu na kutema cheche: “Shilole anatafuta kiki kupitia jina langu, kwanza si hadhi yangu. Siwezi kujibishana na msanii anayetegemea shoo za kwenye vigodoro, akatafute pa kutokea.”
Read more >>

BABY MADAHA AFULIA NA KUBAKI MWEUPE, HANA HATA SHILINGI MOJA

STAA wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ amesema kuwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani umembana kiuchumi kwani kumbi nyingi za starehe zimefungwa kwa hiyo anashindwa kupata pesa.
Staa wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’
Akipiga stori mbili tatu baada ya kuvutiwa waya na mwandishi wa gazeti hili, Baby Madaha alisema kwa upande wake michongo yake mingi ya hela anaipata kupitia kumbi za starehe hivyo kwa sasa fedha haingii kabisa.
“Naomba Mwezi Mtukufu wa Ramadhani uishe maana mtonyo umekata halafu sina namna ya kuingiza fedha zaidi ya muziki hivyo hali si hali kwa sasa jamani,” alisema Baby.
Read more >>

YASEMEKANA BABY MADAHA AENDA KWAO KUTAMBIKA

MAKUBWA! Staa wa filamu na muziki Bongo, Baby Madaha anadaiwa kwenda kijijini kwao kutambika baada ya kuona mambo yake yanamwendea kombo.
Staa wa filamu na muziki Bongo, Baby Madaha.
Akizungumza na mwanahabari wetu, rafiki wa karibu wa Baby Madaha ambaye hakupenda kuanikwa, alisema kutokana na staa huyo kuona mambo hayaendi vizuri hasa kwenye muziki, ameamua kwenda nyumbani kwao Mwanza kwa ajili ya kutambikia mizimu ya kwao.
Baby Madaha.
Alipotafutwa Baby kuhusiana na ishu hiyo, alifunguka:
“Ni kweli niko nyumbani kwetu Mwanza, ni muda mrefu sijaja kumuona mama, kuhusu kutambika hilo ni lazima kwani nikiona mambo hayaendi vizuri, lazima niikumbuke mizimu ya kwetu,” alisema Baby.
Read more >>

BABY MADAHA: SIOLEWI KWA KUFUATA MKUMBO WA WATU WENGINE

STAA wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ amesema anaishi katika staili ya kivyake hivyo kamwe hawezi kuolewa kwa kufuata mkumbo kama ilivyo kwa wasanii wengine.
Staa wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’
Akipiga stori na mwandishi wetu, Baby Madaha alikiri kuwa ana mchumba ambaye ni Joh Kairuki, anampenda sana ila katika suala la kufunga ndoa bado yupoyupo sana kwa sababu haolewi kwa kufuata mkumbo kwani amejifunza kupitia kwa walioolewa na kuachika.
‘Baby Madaha’ akiwa kwenye pozi.
“Nitaolewa nitakapokuwa tayari siyo kwa kufuata mkumbo vinginevyo bora nibakie hivihivi kwa sababu pesa kwangu ndiyo kila kitu, mambo mengine yanafuata,” alisema.
Read more >>

BABY MADAHA NA MENEJA’KE SASA NDOA NOVEMBA

Stori: Gladness Mallya na Hamida Hassan
MSANII wa muziki na filamu Bongo, Baby Madaha na meneja wake, Joe Kariuki wanatarajia kufunga ndoa Novemba, mwaka huu nchini Kenya jijini Nairobi.
Msanii wa muziki na filamu Bongo, Baby Madaha.
Akizungumza na mapaparazi wetu, Meneja wa Baby Madaha, Joe alithitisha mipango hiyo na akasema sasa wanafanya kazi nyingi za muziki mpaka zifike nyimbo 20 ambapo baada ya kuoana zitaanza kutoka mojamoja kwa muda wa miaka minne.
Baby Madaha akiwa katika moja ya kazi zake na meneja wake,Joe.
“Ni kweli tumepanga kuoana, kikubwa ninaandaa nyimbo nyingi ili baada ya ndoa nitasimama muziki na badala yake nitakuwa naachia nyimbo tu,” alisema Baby anayetamba na Wimbo wa Nawaponda.
Read more >>

BAADA YA KUWA NA BIFU LA MUDA MREFU NA DIAMOND SASA BABY MADAHA ASALIMU AMRI NA KUAMUA KUACHA MUZIKI PAMOJA NA FILAMU, SOMA HAPA KUJUA ZAIDI

IKIWA imepita miezi kadhaa tangu anaswe katika mtego  wa kujiuza,  staa wa Bongo, Baby Madaha ametangaza kuachana na sanaa ya muziki na filamu kwa maelezo kuwa amechoshwa na  maisha ya presha. Akiongea  na  mwandishi wetu  juzikati jijini Dar es Salaam, Madaha alisema ishu ile imemsababishia matatizo makubwa ya kifamilia na hata kibiashara, hivyo kujutia mchezo mzima ulivyokuwa.

Alisema filamu anayoisambaza (usisahau kulike page yetu ya mdadisi mambo ka kuclick hapa) kwa sasa na kibao chake cha mwisho kukitoa cha Mr. Dj ndizo zitakazofunga pazia la mambo ya sanaa kwa upande wake.

 “Nimeamua kuachana na sanaa kabisa, siwezi kuishi maisha ya presha yasiyo na uhuru. Nitarudi kwenye fani yangu niliyosomea (hakutaka kutaja), maana naishi maisha ambayo hayana amani kabisa,” alisema.

Read more >>

BABY MADAHA ABADILIKA BAADA YA MTEGO WA KUJIUZA

BAADA ya mwanamuziki Baby Joseph Madaha kunaswa na mtego wa kujiuza uliotegwa na gazeti hili hivi karibuni, mdada huyo anaonekana kubadilika na anadai mgogoro uliojitokeza kati yake na meneja wake, Joe Kairuki kutokana na tukio hilo umekwisha.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni msanii huyo ambaye ni kati ya wasanii wa kike wanaofanya vizuri alisema, tukio lile limefanya ajifunze kitu na kubadilika kwake kumesababisha bosi wake amsamehe na waendelee kupiga mzigo.
“Kweli nimejifunza kutokana na makosa maana kunaswa kwenye ule mtego kumenigharimu sana lakini nashukuru nimesamehewa na mkataba ninaendelea nao, yale yamepita na sasa ni kazi tu,” alisema Baby Madaha a.k.a The Queen of Swaga.

Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger