KUFUATIA tukio la Ustadh Mohamed Said Ngulangwa (36), mkazi wa
Mbagala-Charambe jijini Dar kumchinja mtoto Jamal Salum Ally (12) ambaye
ni mwanafunzi wa darasa la tano kisha na yeye kuuawa na wananchi wenye
hasira, Uwazi kama kawaida yake lilichimba tukio hilo na kubaini mengi,
twende pamoja.
MTOTO AITWA, AENDA
Akizungumza na Uwazi Jumamosi
iliyopita msibani Mbagala juzi, mtoto mmoja (jina lipo) alisema yeye na
marehemu walikuwa wakicheza michezo ya kawaida, mara akatokea ustadh na
kumwita mtoto Jamal.
“Sisi tulikuwa tunacheza, ghafla ustadh akamwita Jamal. We Jamal,
njoo. Kwa vile aliita kwa sauti ya kawaida tulijua anataka kumtuma,
Jamal akaenda mimi nikawa namsubiria ili tuendelee kucheza, kumbe
mwenzangu aliitwa kuchinjwa,” alisema mtoto huyo kwa sura iliyojaa
simanzi.
KISU KIKALI CHATUMIKA
Mtoto huyo aliendelea
kueleza kwa uchungu kwamba, akiwa anamshuhudia Jamal akikutana na
ustadh, alishangaa kumwona mwanaume huyo akimdaka kwa haraka na kisha
kutoa kisu ambapo alianza kumchomachoma nacho na hatimaye kumlaza chini
na kukipitisha shingoni kama anachinja kuku.
“Nilipiga kelele kuwaambia watu, nikatoka kwenda kuwaita watu huku
napiga kelele kwamba Jamal anachinjwa na ustadh,” alisema mtoto huyo
huku akionesha sura halisi ya masikitiko ya ndani ya moyo. Inauma sana!
MAJIRANI WADHANI ADHABU INATOLEWA
Nao majirani
na madrasa ya mtu huyo waliopata nafasi ya kueleza walichojua kuhusu
mauaji ya mtoto huyo, walisema kelele za mtoto Jamal kuomba msaada
zilisikika, lakini waliamini mtoto anapewa adhabu na mzazi wake.
MAMA WA MAREHEMU AFIKA MBIO
Maelezo zaidi
yanasema kuwa, mtoto aliyekwenda kuita watu alifika nyumbani kwa wazazi
wa marehemu na kumkuta mama mzazi ambaye alimpa taarifa.
Mwanamke huyo aliyepewa taarifa hizo, akiwa haamini masikio yake, alitoka mbio na kilio kuelekea eneo la tukio.
Wananchi nao baada ya kusikia maelezo ya mtoto aliyeshuhudia,
waligutuka na kutua eneo la tukio lakini kwa bahati mbaya walikutana na
kichwa kikiwa miguuni mwa kiwiliwili. Lazima umwage machozi!
MBALI NA KIWILIWILI NA KICHWA
Wananchi hao
waliweza kugundua kuwa, kichwa hicho ni cha mtoto Jamal huku pembeni
yake kukiwa na ndoo ambayo walidai muuaji alikusudia kukingia damu (ili
iweje?).
VILIO VYATAWALA, USTADH AJIFICHA
Vilio vilianza
kutalawa eneo hilo, akina mama, marafiki wa marehemu waliangua vilio vya
uchungu baada ya kuuona ukatili huo ambao walisema haujawahi kutokea
katika eneo hilo.
Ilidaiwa kwamba, wakati huo ustadh alikuwa amejificha chumbani kwake
ili kuepuka ‘soo’ lake lakini wananchi walishtukia janja yake na
kutishia kuvunja dirisha ambapo mtuhumiwa huyo alichungulia akiwa na
kisu mkononi kikiwa na mabaki ya damudamu.
WANANCHI WAVUNJA MLANGO, DIRISHA LA USTADH
Bila
kujali kisu hicho, wananchi walivunja mlango na dirisha na kuanza
kumshambulia kwa mawe, kisha wakamchomoa akiwa uchi wa mnyama mpaka nje
huku wakiendelea kumshambulia hadi akakata roho.
BABA WA MAREHEMU NAYE ANALO NENO LA KUSIKITISHA
Naye baba wa Jamal, Salum Ally alipoongea na Uwazi alitoa simulizi ya
majonzi, msikie: “Nilipokea kifo cha mwanangu Jamal kwa huzuni kubwa
sana, sikuamini kama yeye ndiye aliyeuawa kikatili namna ile!
“Nilikuwa narudi nyumbani kutoka kazini, jirani na nyumbani nikakuta
watu wengi, nikahoji kulikoni? Nikaambiwa kuna mtoto amechinjwa na
aliyemchinja ameuawa. Khaa! Nikashangaa!
“Kwa kuwa nilikuwa nimechoka sana, niliona nifike kwangu kwanza ndipo
nirudi kwenye tukio. Kabla ya kutua kwangu, nikakutana na mke wangu
njiani huku akilia, nilipomhoji kuna nini, aliendelea kulia bila kunipa
majibu.
“Ndipo mpangaji mwenzangu akanipasulia kwa kuniambia kwamba mwanangu Jamal amechinjwa mpaka kichwa kutenganishwa na kiwiliwili.
“Nilipatwa na mshtuko mkubwa kwani sikufikiria kama kungetokea tukio
la kutisha kama hilo, hata kama mngekuwa ninyi waandishi mngefanyaje
jamani?
“Nilijivuta hadi eneo la tukio na kukuta mwili wa mwanangu
umeshafungwa kwenye nguo na kuwekwa ndani ya gari la polisi, sikuwa na
nguvu ya kuangalia sura yake kwa uchungu nilioupata kwani ndiyo mtoto wa
kwanza,” alisema Salum.
USTADAH ALIPANGA MAUAJI?
Uchunguzi wa gazeti
hili ulibaini kuwa, ustadh huyo alijiandaa kutekeleza mauaji hayo kwa
vile aliandaa kisu na ndoo kwa ajili ya kukingia damu ya mtoto huyo kwa
kile watu walichodai alitaka kuinywa.
POLISI MZIGONI
Baadaye taarifa zilienea maeneo
yote ya Jiji la Dar hususan Mbagala-Charambe na polisi walitua eneo hilo
na kuchukua miili ya marehemu wote wawili na kupelekwa chumba cha
kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Temeke.
Pale hospitalini, madaktari walitumia saa mbili kichwa cha mtoto Jamal na kiwiliwili.
USTADH ATAJWA KUTOKUWA NA AKILI
Mdogo wa Ustadh
Mohamed aliyekuwa msemaji wa familia, Daudi Ngulangwa alisema marehemu
kaka yake aliwahi kupatwa na ugonjwa wa akili mwaka 1995/96 kisha
kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kutibiwa na akapona.
MAZISHI YAO
Marehemu Jamal alizikwa Jumamosi iliyopita katika Makaburi ya Mbagala-Charambe jijini Dar (Uwazi lilikuwepo).
Ustadh Mohamed, yeye alizikwa siku hiyohiyo kwenye Makaburi ya Manzese jijini Dar es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment