Elizabeth
Michael’Lulu’ ambaye anakabiliwa na kesi ya mauaji bila kukusudia ya
Steven Kanumba anatarajia kuanza kujibu mashitaka yake kwa mara ya
kwanza Februari 17 mwaka huu katika Mahakakama Kuu Tanzania Kanda ya Dar
es Salaam.
Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya kesi za mauaji na bila kukusudia iliyotolewa na Mahakama Kuu kwa kanda ya Dar es salaam,kesi ya hiyo ya Lulu itasikiliza mbele ya Jaji Rose ratiba hiyo inaonyesha kwamba mshtakiwa akisomewa mashtaka na kujibu,mahakama itapanga tarehe ya kusikiliza maelezo ya awali dhidi ya kesi hiyo.
Lulu ambaye Januari 29 mwaka 2013 aliachiwa kwa dhamana baada ya kesi hiyo kubadilishwa hati ya mashitaka kutoka kwenye kesi ya mauaji kwenda mauaji ya bila kukusudia na Lulu kupata dhamana hiyo.
Baada ya Jaji Zainabu Mruke kutoa masharti ya dhamana kwa mshtakiwa huyo ambapo wakili wa utetezi Peter Kibatala baada ya kuwasilisha maombi ya dhamana kwa hati ya dharula chini ya kifungu cha 148 kidogo cha (1) na cha (2) cha Mwenendo wa Sheria ya Makosa ya Jinai (CPA).
Katika kesi ya msingi inadaiwa kuwa Lulu Aprili 7 mwaka 2012 katika eneo la Sinza Vatican jijini Dar es Salaam,Mshtkiwa alimuua Kanumba bila kukusudia.

No comments:
Post a Comment