| NB-Picha haihusiani na tukio katika habari |
Mwalimu
wa shule ya msingi Mwang’osha kata ya Nyamalongo wilaya ya Shinyanga
Vijijini Christipian Mafuru (24) amefariki dunia baada ya kujinyonga
kwa kutumia kamba ya katani katika choo kilichopo nyumbani kwake.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mwalimu mkuu wa shule hiyo Frida Maleko amesema
marehemu Mafuru amegundulika akiwa amejinyonga juzi majira ya saa tisa
na nusu alasiri.
Amesema
baada ya mwalimu huyo kutoonekana shuleni hapo kwa muda mrefu
walijaribu kumpigia simu marehemu bila mafanikio na kuamua kuondoka na
walimu wenzake kwenda nyumbani kwake na kukuta mlango umefungwa huku
simu ikiita ndani bila ya kupokelewa.
Maleko
amesema walichukua jukumu la kuvunja dirisha na mara baada ya
kufanikiwa kuingia ndani walikuta ujumbe wa maneno mezani uliokuwa
umeandikwa na marehemu ukisomeka kuwa.......
"MSONGO WA MAWAZO UMENILAZIMU NIFANYE HIVI,POLENI SANA WALIMU WENZANGU,SAMAHANI WAZAZI WANGU,KWA HERI MWANANGU REY"
Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Evarist Mangalla amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

No comments:
Post a Comment