
Akizungumza na paparazi wetu kuhusu ishu hiyo, Malingo alisema kwamba akiwa anaoga alisikia sauti ya vishindo vya mtu aliyekuwa akitembea.
Kiongozi huyo wa UWT, alisema baada mtu huyo kusimama aliamua kumchungulia kupitia tundu la funguo ndipo alimuona Asna akianua nguo za ndani na nyingine ambazo zilikuwa mbichi na kuzisunda kwenye pochi na mfuko wa rambo.
“Kama unavyoonaniko na khanga moja tu, nilikuwa bafuni naoga nikasikia vishindo, nilipochungulia kwenye tundu la funguo nikamuona huyu msichana anaanua nguo za mgonjwa aliyelazwa Hospitali ya Mkoa ambazo nimetoka kuzifua sasa hivi, nikajifunga khanga na kutoka nje na kuanza kumfukuza huku nikimwitia mwizi, cha ajabu na yeye alipaza sauti kwamba hakuwa mwizi bali alinifumania na mume wake,” alisema Malingo.
Malingo aliongeza kuwa, kufuatia mayowe ya mwizi aliyotoa, watu walijitokeza na kuanza kumpa kichapo msichana huyo huku wengine wakitaka kumchoma moto.
Wakati dada huyo akiendelea kula kichapo alitokea paparazi wetu aliyewapigia simu askari wa kike waliokuwa doria ambao walifika na kumtia mbaroni msichana huyo.
Askari hao walimpeleka Kituo Kidogo cha Polisi Kata ya Mji Mpya akafunguliwa jalada la kesi namba MJ MPY/RB/18/2014 WIZI kisha kupelekwa mahabusu ya kituo kikuu. Aidha, Bi. Malingo alisema kwamba hivi karibuni amekuwa akiandamwa na vibaka nyumbani kwake kwani wiki kadhaa zilizopita wezi walivunja dirisha la chumba cha kijana wake Ally na kuiba redio ya ya shilingi 800,000, deki ya 200,000 na simu ya shilingi 100,000.
No comments:
Post a Comment