Suala la posho limezidi kuwa kaa la moto katika vikao vya Bunge la Katiba vinavyoendelea mjini Dodoma leo, hali iliyomlazimu mwenyekiti wa muda, Pandu Ameir Kificho ateue timu maalum ya watu 6 kutazama jinsi ya kuboresha viwango vya posho hizo.
Timu hiyo inatarajiwa kuyachunguza kwa undani
mahitaji ya wajumbe wa Katiba, kisha kuisaidia serikali kutafuta jinsi
ya kuongeza posho hizo.
Wajumbe wa timu ya posho ni pamoja na mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Uratibu na Bunge), William Lukuvi.
Wengine ni mjumbe wa asasi zisizo za kiserikali
Paul Kimiti, Mbunge wa Peramiho Jenister Mhagama (CCM) na wajumbe wa
Baraza la Wawakilishi Asha Bakari na Mohamed Aboud Mohamed.
Huku hayo yakiendelea Dodoma, Katibu Mkuu wa
Chadema Dr Wilbrod Slaa amedai kuwa posho wanayopewa
wajumbe ya Sh 300,000 kwa siku inatosha kabisa, “kwa kuwa hata
wafanyakazi wengine wa serikali wanapokea mshahara wa laki tatu mwisho
wa mwezi.”
Mwenyekiti Msaidizi wa CUF, Julius Mtatiro anaunga
mkono mtazamo huu. Katika waraka wa wazi aliouweka kwenye ukurasa wake
wa Facebook, Mtatiro anaandika:
“Shilingi laki tatu tunazopewa kwa siku zinatosha
kabisa, ambaye hazimtoshi aongeze za kwake [ama] aondoke Dodoma ili
kupisha wanaoweza kutunga katiba kwa posho ya Sh 300,000 waendelee.”
No comments:
Post a Comment