
AMANDA
Poshi mwigizaji wa filamu Bongo amesema kuwa kwa sasa yupo single hana
mchumba wala mume bali anasubiri atokee mwanaume mwenye sifa ambazo
kaziweka wazi, endapo atatokea mtu wa namna hiyo atajikwalia ushindi kwa
kumpata yeye na kuwa mke wa maisha yake.
.

Amanda Poshi akiwa katika pozi

“Nahitaji
mwanaume mchakalikaji, mishemishe za mjini anazijua, anijali na
kunipenda zaidi sipo tayari kuolewa na mwanaume asiyejielewa, mtu
mwelewa ambaye hauwezi kupishana Kiswahili na kuzua balaa la ugomvi
siwezi bab,”anasema Amanda..

Amanda Poshi akiwa katika pozi

Moja ya masharti yake mengine ni pamoja na mwanaume ambaye atakuwa tayari kumuoa awe tayari kumruhusu kuendelea na kazi ya uigizaji asimzuie kwani itakuwa ndio sababu ya kutengena kwao, mtu ambaye atakuwa tayari kwa hayo atampatia zawadi ya kumzalia watoto wawili kwa maisha yao

No comments:
Post a Comment