Tovuti ya Times Fm imefanya mahojiano
‘exclusively’ na Robina Nicholaus, msichana aliyeshika nafasi ya kwanza/
aliyeongoza kitaifa (Tanzania One) kwenye matokeo ya mtihani wa kidato
cha nne mwaka 2013.
Robina, mwenyeji wa wilaya ya Bunda mkoa
wa Mara ambaye alikuwa anasoma katika shule ya wasichana ya Marian,
akiwa na ndoto ya kuwa daktari wa watoto amejibu maswali kumi muhimu na
majibu yake yanaweza kuchukuliwa kama mfano wa kuigwa kwa wanafunzi
walioko shuleni ambao wanakumbwa na changamoto kadhaa, na wazazi
wanaowapeleka watoto wao shule.
Ulifanya nini ghafla ulipopata taarifa kuwa umekuwa wa kwanza Tanzania nzima, na je, ulitegemea?
Nilipopata matokeo kwamba nimekuwa wa
kwanza, kwanza nilifurahi sana na kilichobaki zaidi ilikuwa ni
kumshukuru Mungu kwa sababu yeye ndiye kayawezesha yote. Nilihisi kama
kupaa vile…nilifurahi sana halafu my mom alikuwa pale… alikuwa analia
akaniinfluence na mimi machozi yatoke, I was very happy yaani.
Sikutegemea kuwa wa kwanza lakini nilikua na uhakika wa kufanya vizuri
kwa sababu niliplan kufanya vizuri.
Kama msichana ulifanya nini kuzivuka changamoto za kimasomo na kufanikisha kwa kiasi kikubwa?
Safari ya taaluma ni ndefu ndio, kwenye
safari ya masomo kuna changamoto za hapa na pale, ambapo mara nyingi
wasichana waga tunafanya maamuzi ambayo sio sahihi. Lakini kwangu mimi
nimeweka interest yangu sana kwa wazazi. Kwa hiyo nilikuwa open kwa
wazazi na kuwaomba ushauri wa hapa na pale nifanye nini. Na katika vyote
nilivyokuwa nafanya ni kufanya kile kitu ambacho hakiwezi kusubiria
kwanza ambacho ni masomo. Kwa hiyo naweka juhudi pale ili ukishafanya
kila mtu ajue kwamba umefanya.
Ilikuwa mbaya sana kwenye kusoma hasa
form three ambapo nilianza kushuka and all that. Kwa hiyo wazazi pamoja
na walimu pia walikaa na kuweza kunisaidia na mimi mwenyewe nilikuwa
tayari kusikia ushauri wao na kuweza kusoma kwa bidii zaidi ili niweze
kupata ile nafasi yangu niliyokuwa naipata toka nianze.
Nini kilichofanya ushuke kimasomo wakati huo?
Kilichofanya nishuke ni ile kupoteza
malengo na juhudi zangu, na pia kuona kwamba vitu vinaanza kuwa vigumu
halafu kuweka hiyo kwenye akili kwamba hicho ni kigumu siwezi kukifanya.
Lakini nilipoamua kuweka juhudi na kuona kwamba ni vitu vya kawaida
kwamba navyozidi kukua na vitu vinazidi kuwa vigumu na natakiwa nitafute
njia ya kuvi-overcome, ndo hivyo nikaweza kufanikiwa.
Ratiba yako ya siku ulipokuwa shule kwa ujumla wake ilikuwa vipi na muda gani ulikuwa unajisomea?
Asubuhi nilikuwa naamka mapema kabla ya
time table ya shule haijaanza kwa sababu tunatakiwa tuamke mapema kwenda
misa kwenye saa kumi na moja hivi. Kwa hiyo naamkaga kwenye saa tisa
najiandaa naenda darasani kwa sababu siwezi kusoma usiku kwa sababu
usiku nakuwa nimechoka, kwa hiyo my extra time inakuwa asubuhi ambako
I’m still fresh.
Nasoma then ikifika muda wa misa naenda
kusali. Nikitoka kusali kuna kazi ndogo ndogo za kufanya kujiandaa na
time table ya school and all that. And my free time ile mchana nikitoka
darasani kuanzia saa nane, nakuwa nimepanga nini natakiwa nifanye, ni
somo gani natakiwa kulisoma at that time ambapo ni saa nane mpaka saa
kumi na nusu. Ambapo ni muda wa concentration, kama kuna kitu ambacho
sijaelewa naenda kuwafuata waalimu kwa sababu wanakuwa wapo at that
time. And kuna some free time kama ile break time, ni kuanzia saa nne na
dakika 40 mpaka saa tano na robo, pale hauwezi kusema unatake breakfast
all the time, unatake breakfast for a short time halafu nyingine
inabaki unaweza kufanya maswali matano ya physics. Yaani every little
time ambayo unaweza kuipata, you don’t let it go to waste tu,
una-utilize.
Marafiki ulionao wanaweza kusaidia kukupandisha au kukushusha. Wewe ulikuwa na marafiki wa aina gani?
Marafiki wangu nimewachagua kwa
category..yeah (anacheka), ikifika muda wa kusoma nakuwa na mtu ambaye
najua atanisaidia, kwa hiyo nilikuwa na rafiki yangu anaitwa Sarafina
amekuwa wa nne. Alikuwa ananiinfluence sana kusoma, huyo ni wakati wa
kusoma, kwenye academics namfata yeye.
Ikifika wakati wa social siwezi kumfata
sarafina kwa sababu she is not that social, yeye yuko kama mimi we are
not that social, kwa hiyo ninaye social friend. Pia ikifika muda wa
kuspend, I have an economical friend. Ambaye I’m sure nikikaa nae nikiwa
naspend siwezi kwenda beyond my budget. Kwamba siwezi kufulia. Kwamba
we are all in the same status, same friends, yeah.
Ni kitu gani kilikuwa kinakuboa sana shuleni na kukunyima furaha muda mwingine?
Kitu ambacho kilikuwa kinaniboa sana,
ikifika wakati ambapo kwa mfano watu wachache kwenye darasa wamefanya
kosa halafu sasa mnakuwa included as a whole class halafu mnapata
adhabu. Hiyo adhabu directly itaharibu time table yangu ya kusoma. Kwa
hiyo badala ya kusoma nafikiria ningekuwa nasoma physics, I’m either
slashing an area..yaani hiyo ilikuwa inaniboa sana yaani.
Ulishawahi kuitwa ‘Msongo’ au majina kama hayo? Ulikuwa unaichukuliaje na je, ilikutenga na marafiki zako?
Yeah, msongo…kauzu. Yeah mimi naipenda
hivyo kwa sababu nafanya nachotakiwa kufanya ambacho ni kusoma. Hiyo
haikunitenganisha na marafiki zangu.
Vuta taswira, je, ingetokea ukapata
division Zero na kuwa wa mwisho Tanzania nzima ungefanyaje? Na
unawashauri nini waliofeli kwa kiasi hicho?
Kama ningepata zero, kwanza
ningefikiria…na ningekuwa very disappointed kweli, lakini pia
ningefikiria kuhusu kujipa second chance, ningeenda kusoma tena.
Kwa waliofeli ningependa kuwashauri
wasikate tamaa hata kidogo and wajipe second chance. Kwa wengine pia
ambao wana vipaji vyao wanaweza kuviendeleza. But pia kwa kuwa elimu ni
muhimu..ku-reseat pia ingekuwa ana option.
Robina Nicholaus ni msichana wa aina gani?
Robina ni mtu mkimya lakini mcheshi pia.
Nisingependa nikae na mtu halafu nikawa kimya just because ni mkimya...
I will try kuchekesha, and of course I’m funny anyway.
-via timesfm
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment