
STAA wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ hivi karibuni alijikuta akigeuka kituko kwa watoto yatima kutokana na mavazi ya ‘kihasara’ aliyokuwa amevaa na kulazimika kujistiri na mtandio kiunoni.
Nisha akiwa na timu yake (Team Nisha), walikwenda kutoa msaada katika Kituo cha Mwana Orphans Centre kilichopo Vingunguti, jijini Dar na walipofika walijishangaa kwa kuwa watoto hao walikuwa wamevaa mavazi ya heshima.
“Mh! Imebidi nijistiri kidogo na mtandio lakini kimsingi nimeguswa na watoto hawa kwa sababu na mimi ni yatima na haya maisha nimeyapitia hivyo kila mwisho wa mwezi tutakuwa tukitembelea kituo hiki na kuwaletea mahitaji muhimu,” alisema Nisha.
Nisha na wenzake walitoa misaada ya vifaa mbalimbali vikiwemo sabuni, vyakula na vinywaji huku mmoja wao aliyekuwa na ‘bethdei’ akikata keki na kula na watoto hao.

No comments:
Post a Comment