Najua
wengi mtakimbilia hapa mana'ke wanawake na ndoa ni kama vile inzi na
kipindu-pindu au kashata na gahawa/kahawa anyway sitokuhakikishai kuwa
nitakachokuambia kitafanya kazi kwani inategemea zaidi na mpenzi wako,
malezi, mazingira,akili yake (yaani how open minded he is) na aina ya
maisha yake.
Nakumbuka
siku moja nilikuwa na marafiki zangu fulani (well wadada nimesoma nao
pamoja) mmoja akasema kuwa "James lazima nimfanye anioe" nikajiuliza kwa
sauti kuu huku na cheka (kidhani ni utani) unamfanyaje mwanaume
atangaze ndoa? Ninavyojua mimi ni kuwa mnalizungumzia swala zima kisha
mnasikiliziana kama nyote mna nia moja then siku moja mpenzi (mwanaume
ndio anatangaza ndoa/posa) si ndio....hiyo kisasa.
Ya
kizamani ilikuwa binti unajitahidi kuwa masafi na mwenye tabia njema
kisha mwanaume anakuona kuwa wewe ni "ndoa type" then anakuja kwa wazazi
wako kuposa kama sio wazazi wake wanakupenda kisha wanawashawishi
wazazi wako wakubali uolewe na mwana wao wa kiume alafu from there ndio
unaanza kujifunza kama sio kujilazimisha kumpenda aukumzoea kama mume
wako ajae.
Kwa
bahati siku hizi tunakuwa kwenye mapenzi na mapendo, kisha tunafanya
nusu na robo kama sio yote yanayofanywa kwenye ndoa lakini jamaa
halitangazi ndoa wala nini na wewe unahisi siku zinakwenda na huna
mpango wa kuzaa nje ya ndoa.
Mwenyewe
unajitahidi kumpena na kumuonyesha mapenzi yako, unaongeza ubunifu
kitandani, unampa uhuru/nafasi yake anapohitaji kwenda kulewa
(humfuatilii), mnakwenda kwenye sherehe za ndoa una-comment jinsi
ambavyo siku moja ungependa naninyi mfanye hivyo.....yaani unampa dalili
zote kuwa wewe ni a good wife, lakini Njemba haitangazi ndoa....!
Inaweza
ikafikia wakati ukahisi uvumilivu umekushinda na umechoka kupotezewa
muda na hivyo kuchukua uamuzi na kumwambia kama kweli unanipenda
ungefunga ndoa na mimi siku nyingi so ama unanioa ktk wiki moja au
uhusiano umekufa......hapo lazima atatangaza ndoa ili asikupoteze ikiwa
kweli anakupenda au anajua unampenda na hakuna mtu atakae mpenda kama
wewe ila tatizo la hii kitu ni kuwa wewe mwanamke ndio unaonekana
Desperate kuolewa hivyo unakuwa umelazimisha......ni bonge la noma!
Nikirudi
nitakupa mbinuz za kumfanya mshikaji atangaze ndoa na kuifanya itokee
sio mnakuwa wachumba kwa miaka 3 wakati tayari mmeishi pamoja kama
wapenzi kwa miaka 5.....it's boring bana.
Usicheze mbali.
Utachumbiwa lini.........?
Wengi
tunaamini kuwa matunda ya mapenzi ni ndoa na sote tunatambua kuwa ndoa
ni jambo zuri, la heshima (wengi wanafeli hapa), busara na chanzo cha
familia bora (japo kuwa mimi siamini sana hapa). Kinachosikitisha ni
kuwa huu uamuzi huwekwa wazi na mwanaume na sio mwanamke hata kama wewe
ndio unataka kuolewa yaani umefika bei n aunajua kabisa Haruna ni the
one lakini Haruna mwenyewe khabari hana (well kama haruna (muislamu) na
haja adopt tamaduni ya watu na yuko karibu au juu ya miaka 25 lazima
atatangaza ndoa kwa mujibu wa dini yake) hivyo bora nitumie jina la
Jonathan hahahahaha.
Nimeona
hapo chini M2 anasema wanawake tuwe wagumu kutoa K kwani akisha onja
hataki tena, nasikitika kusema kuwa swala la ndoa ni zaidi ya K na
vilevile swala hili linachanganya kiaina. Wakati mwingine mimi huwa
naamini kabisa kuwa ndoa ni mapenzi na uamuzi (labda kwa vile kila
nilietoka nae kama mpenzi alitangaza ndoa), wengine wanadai kuwa ni
bahati na baadhi wanasema ni lazima kama ilivyo ktk kuzaliwa na kufa, si
unakumbuka sherehe 3 hapa duniani kuwa ni kuzaliwa, kuolewa/oa na kufa.
Watu
nitakao walenga ni wale ambao wako tayari kwenye uhusiano na
wanapendana lakini wanataka wapenzi wao wawasapuraizi kwa pete ya
uchumba au hata kwenda kutambulishwa kwao kuwa wao ndio wapenzi wa
kudumu.
Mpenzi
akifika bei unamjua tu, wala huitaji vithibitisho si ndio jamani?
Lakini mapenzi yake kwako sio tiketi ya yeye kukufanya wewe wa milele
hivyo suibweteke nakusubiri siku akijisikia atangaze ndoa wengine mpaka
uwaonyeshe kuwa "U can live with or without them" ndio wanajisogeza
zaidi, sasa fuata haya yafuatayo:-
1-Ni
mwiko kumkutanisha/tambulisha kwaa wazazi wako au kumpa namba ya simu
ya nyumbani kama sio ya baba na mama (ya wazungu waachieni wenyewe)
haruhusiwi kuwazoea bila kuji-commit. Kumbuka kuwa mwanaume anatakiwa
kulifanyia kazi hili na kuhakikisha kuwa anakutana na wazazi wako
nakujitambulisha ikiwa tu pete iko kidoleni na mnakwenda huko
kutambulisha uchumba rasmi nakufuata taratibu nyingine za mahari, barua
n.k. sio mmekutana leo kesho yuko sebuleni angalia Tv au kucheza na
wadogo zako kama sio kuwapeleka kwenye manunuzi pale soko mjinga au
kwenye maonyesho ya saba-saba.
Kama
kwa bahati mbaya tayari amekwisha kutana na wazazi wako kabla ya makala
yangu hii basi hakikisha hapati tena nafasi hiyo,mpaka kuwepo na pete
au hata yeye kuandika barua nakulipa mahali nusu na robo (mana'ke sio
wote wanaamini ktk pete).
Ikitokea
shughuli kubwa kwenye Ukoo wenu kama vile sherehe za ndoa au Msiba
hakikisha unakwenda mwenyewe bila yeye, ofcoz unamwambia nini nimetokea
(msiba)au kinakwenda kutokea(ndoa) na akiomba kushiriki au kwenda na
wewe mwambie ungependa awepo lakini hudhani kuwa ni wazo zuri kwani
utakuwa busy sana (hutokuwa na muda wa kuwa pamoja kama wapenzi) na sio
hivyo tu bali unajaribu kum-save na too much hassle.....hapa atakuona
wewe ni wa maana sana nakuna uwezekano mkubwa siki za karibuni akataka
uwe wake wa daima milele(Daima).....Usisahau kuwa hayuko pale kupendwa
na ndugu zako na wala haitaji kupenda na kuzoea nyumbani kwenu.
2-Kamwe
aah ni marufuku kuhamia kwake au yeye kuhamia kwako ikiwa kila mmoja
wenu anajitegemea (anaishi kwake), wengi hukimbilia ku-move in wakihofia
wapenzi wao kuchukua watu wengine na kulala nao.....skia wewe, achakuwa
tegemezi kihivyo (emotional) utakimbiwa, kila mtu anahitaji nafasi yake
time to time, swala la kulala na mtu mwingine kama lipo basi anaweza na
mtu huyo hotelini, nyumba za kulala wageni au hata ofisini wakati kila
mtu katoka....swalamuhimu ni mapenzi ya dhati na uaminifu.
Ikiwa
ulihamia kwake ili ukamuonyeshe umuhimu wako kama "mke" yaani kupika,
kusafisha, kupiga basi, kumpangia nguzo shati na tai nzuri kwa ajili ya
kazini n.k. na bado Njemba haina dalili yakutangaza ndoa basi ni wakati
wa kuhamia kwako peke yako kama sio kurudi kwa dada/wazazi, na kumbuka
unapo hama bakiza kachupi kako kadogo ambako anakapenda kukaona maungoni
mwako.
Ukihamia
kwa mpenzi wako kabla ya kuchumbiwa, itamafanya ajisahau navilevile
atakujua kwa sana yaani mambo mengine ulitakiwa uyafanye baada ya miaka 5
yandoa wewe unayafanya kabla hata ya uchumba na nina kuhakikishia ndoa
haitoangazwa unless baba na mama'ke wamwambie "hey bwan' mdogo unataka
tufe kabla hatujamuona mkwe na mjukuu "ndio atatuma posa?
Yaleyale......!
Kuhamia
kwake kunaruhusiwa ikiwa tu ametangaza ndoa na maandalizi ya ndoa
yameanza (tunaita trial), alafu mwezi mmoja kabla ya ndoa unarudi
kwenu....sio kwako....kwenu kwa wazazi au ndugu.
3-Ni
mwiko kujifananisha ninyi na pea inayo au iliyofunga ndoa hivi
karibuni, yaani wewe unatakiwakua "nunda" when it comes kwenye maswala
ya ndoa au uchumba wa watu wengine, hasa kama yeye anaonyesha kutokuwa
na habari (kawaida wanaume huwa hawana habari wala wivu) basi na wewe
kuwa kama yeye.
Siku
umeenda kumtembelea Mpenzi amabe kafika bei ila swala la ndoa halipo
eti mpaka ajenge nyumba......lini? (kumbuka hakuna kuishi pamoja mpaka
achumbie)ukiwa unaongea na rafiki yako amabe kafunga doa hakikisha
unasema sentensi za kuponda ndoa kwa sauti ili mpenzi asikie tena kwa
kunogesha muulize "hivi inakuwaje unaweza kuishi na mtu yuleyule kila
siku iendayo kwa Mungu?" Mimi sidhani kama nitaweza, nahisi itakuwa
boring"......hehehe kwa yote unayomfanyia nakumridhisha kitandani, kwa
jinsi unavyompenda na kumjali alafu anasikia hivyo.....yaani akili
itamjia Njemba nyingine zinaweza niwahi hapa......ataenda itafuta pete
ktk siku zijazo, wewe subiri tu.
Hakikisha
unayasema yote hayo kuwa unajua kabisa anakupenda kwa dhati na maisha
bile wewe ni bora kifo.....mana'ke ukisema haya kwa player ujue kashinda
na atakung'ang'ania na pete usiione alafu anaenda kuoa mtu mwingineee.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment