MKURUGENZI wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga
Pepeta’, Asha Baraka ‘Iron Lady’ amewaasa wasanii wanaofanya kazi za
sanaa nje ya nchi wawe na desturi ya kurejea nyumbani mara kwa mara ili
wasisahaulike kwa mashabiki wao.
Akizungumza na gazeti katika mazishi ya msanii Amina Ngaluma
aliyefariki wiki iliyopita nchini Thailand, aliwataka wasanii wote
wanaofanya kazi za sanaa nje ya nchi wawe wanarudi nyumbani maana kifo
hicho kimetoa somo kwa upande mwingine.
“Unajua Amina amekaa sana nje ya nchi bila kurudi nyumbani na kufanya
shoo katika kumbi za nyumbani ndiyo maana hata wanamuziki wachanga
wanashindwa kumtambua vizuri, wabadilike,” alisema Asha Baraka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment