HATIMAYE NDOA YA WASANII WA KAOLE YAJIBU

WASANII wa filamu zao la Kaole, Mariamu Athuman ‘Kalunde’ na Khely Ahmed ‘Niko’ ndoa yao imejibu ambapo hivi karibuni wamepata mtoto. Akizungumza na gazeti hili, Kalunde alisema ana furaha ya ajabu kufuatia kumpata mtoto wa kike na anamshukuru Mungu kwani alijifungua salama bila matatizo.
Msanii wa filamu zao la Kaole, Mariamu Athuman ‘Kalunde’ akiwa na mwanae aliyejifungua hivi karibuni.
“Namshukuru Mungu sana kwa kutupatia mtoto wa kike mimi na mume wangu, huyu mtoto ameongea furaha ndani ya ndoa yetu kwani ameongeza familia,” alisema Kalunde.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger