MAKUBWA! Baada
ya kujichora tatuu mbalimbali mwilini mwake, kuonesha amechizika
kimalovee, mwigizaji Lungi Maulanga amechora moja yenye sura ya mpenzi
wake ambaye hakutaka kumtaja.
Mwigizaji wa Bongo Muvi, Lungi Maulanga.
Akipiga
stori na mwanahabari wetu, Lungi alisema kuwa ana tatuu 12 mwilini
mwake ambazo alizichorea pande za Dubai alipokuwa ameenda kutembea
lakini mahaba niue ndiyo yalimtuma achore hiyo yenye muonekano wa
mchumba’ke.
“Tatuu
zina maana lakini moja nimemchora mpenzi wangu na hata nikikutana na
mwanaume yeyote anajifanya ananihitaji ajue kabisa ninaye nimpendae
zaidi kwani tatuu hii siwezi kuifuta,” alisema Lungi ambaye amechafuka
tatuu katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye titi, paja na kiuno.
Mwigizaji wa Bongo Muvi, Lungi Maulanga.
No comments:
Post a Comment