Mtu
mmoja ambaye alikuwa akishiriki vitendo vya wizi alijikuta akimpa Yesu
maisha yake hapo jana mara baada ya kukimbilia kanisa la The Oasis
Healing Ministries lililopo nyuma ya jengo la Ubungo Plaza jijini Dar es
salaam, mara baada ya mwizi huyo kukimbilia kanisani hapo akisalimisha
maisha yake baada ya kuiba alikotoka.
Mwizi
huyo ambaye hata hivyo GK haikupata jina lake, mara baada ya kukimbilia
kanisani hapo, aliweza kuhubiriwa neno la Mungu ambalo alilipokea na
kumkubali Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake na kuahidi kuendelea
kumshika na kumkiri Yesu, hata kokote atakapopelekwa na jeshi la polisi
ambao walifika kanisani hapo kumchukua mwizi huyo.
Tukio
la mwizi huyo kumpokea Yesu lilipokelewa kwa shangwe na waumini wa
kanisa hilo ambao walishindwa kuzuia furaha hiyo hata mwizi huyo
alipopandishwa kwenye gari ya polisi, ambapo mchungaji alimuombea huku
mwizi huyo akionekana mwenye utulivu.

Gari alilopakizwa mwizi huyo





No comments:
Post a Comment