DIVA wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameziomba mamlaka
zinazosimamia maadili ya filamu nchini ziwaruhusu wasanii waigize nusu
utupu ili kuendana na soko la kimataifa.
Akitetea hoja yake mbele ya paparazi wetu, staa huyo aliyeitendea haki
filamu ya Foolish Age alitolea mfano Tamthiliya ya Shuga iliyomtoa
Lupita Nyong’o ambayo alicheza akiwa nusu utupu.
“Wanasema hatufuati maadili wakati kuna muvi ambazo zipo theatre na watu wanaangalia hazina maadili, wao wanataka tufanye vitu kwa kudanganya wakati sasa hivi tuko dunia ambayo tunatakiwa tuweke vitu wazi, wasibane sana,” alisema Lulu.
No comments:
Post a Comment