Umaarufu wake uliongezeka zaidi pale alipokamatwa na madawa huko Afrika Kusini, jambo lilomfanya anyee debe kidogo kabla ya kuachiwa na kurudi uraiani kwa mbwembwe zote. Ikapita miezi michache akarudi bongo huku akiwa mtu huru kabisa.
Wiki chache zilizopita Agnes aliamua kurudi sauzi kwa yule mchumba wake aliyekoswa koswa kukamatwa nae na madawa ya kulevya na tetesi zinasema kua alirudi sauzi kumpa taarifa bwana wake huyo kua yeye kwa sasa ni mjamzito.
Tetesi hizo zimethibitishwa jana pale Agness alipoamua kuweka picha yake
Instagram na kuandika " Mama Kijacho " Ikimaanisha kua siku si nyingi
ataingiza kiumbe kipya duniani. Inadaiwa kua Mchumba wake huyo kwa
furaha aliyoipata baada ya kupewa taarifa hizo aliamua kumvalisha pete
ya uchumba kabisa.
Habari BongoClan tulizozipata kutoka kwa ndugu wa karibu wa Agness ambae
hakutaka kutajwa jina lake ni kua Mchumba wake huyo anaplan za kuja
Bongo kutoa mahari kabisa ili baada ya Masogange kujifungua wafunge
Pingu za maisha.
Ndugu huyo aliendelea kusema kua Pete ya uchumba aliyovalishwa Masogange
ina gharama ya shilingi milioni 16 za kibongo. Tunapenda kutoa hongera
kwa Agness na mchumba wake kwa kuamua kuchukua maamuzi mazuri ya kupata
mtoto kwani mastar wengi wanaogopa kuazaa kwa kuhofia kushuka umaarufu.
BongoClan
BongoClan


No comments:
Post a Comment