Sherehe hiyo ilifanyika Jumamosi iliyopita katika Ukumbi wa Mwika, Sinza
jijini Dar ambapo pamoja na zawadi nyingine, maharusi hao waliondoka na
shilingi millioni tatu, fedha taslimu.
Mpango mzima wa kuwamwaga ‘minoti’ uliongozwa na muigizaji Yobnesh Yusuf
‘Batuli’, Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’,
Jacob Steven ‘JB’, Kulwa Kikumba ‘Dude’ na wengineo ambapo mwishoni
hesabu ya jumla ilitimia shilingi milioni tatu.
Kwenye sherehe hiyo, hawakuonesha utengano, hawakujali kama ni memba wa
Bongo Movie au Shirikisho la Filamu Nchini (TAFF) lililowakilishwa na
rais wake, Simon Mwakifamba ambaye muda wote alionekana mwenye furaha.
Mbali na Steve Nyerere, JB, Batuli na Dude, mastaa wengine waliohudhuria
sherehe hiyo ni pamoja na Issa Mussa ’Cloud 112’, Elizabeth Michael
‘Lulu’, William Mtitu, Single Mtambalike ‘Rich’, Yvonney Cherry
‘Monalisa’, Suzan Lewis ‘Natasha’ na wengine wengi.

No comments:
Post a Comment