WASANII wa
filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel amesema hivi karibuni aligongana uso
kwa uso na Ivon Bigilwa ambaye anadaiwa kumchana kwa chupa mkononi na
kesi hiyo inaendelea katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Msanii wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel akliwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar.
Aunty alisema hayo juzi Jumatatu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
jijini Dar es Salaam mbele ya hakimu Agustina Mbando, akikanusha taarifa
ya wadhamini wa Ivon, Christopher Mwaseba na Anthon Mwaseba walioiambia
mahakama kuwa mtuhumiwa alikuwa nyumbani akimuuguza mama yake.
Ivon Bigilwa aliyemchana Aunt kwa chupa.
Msanii huyo alisema wadhamini hao wanaidanganya mahakama kwa kuwa hivi
karibuni alikuwa nchini China na aligongana naye uso kwa uso.
Kutokana
na hilo, Hakimu Mbando aliwaonya wadhamini hao kwa kuidanganya mahakama
na kuwataka wampeleke mtuhumiwa huyo mbele ya mahakama hiyo Juni 10,
mwaka huu.
No comments:
Post a Comment