MGANGA WA DIAMOND AIBUKA TENA, HII NI BAADA YA MSANII HUYO KUPATA TUZO 7


Yule mganga maarufu wa mastaa nchini ambae

aliwahi kutangaza kuwa amekuwa na ukaribu na

mwanamuziki Diamond ameibuka na kusema

kuwa tuzo hizo saba alizozipata zinamaana

kubwa sana kwenye kazi zake anazozifanya.



alisema" Niliongea na Diamond wiki moja kabla

ya shoo nikamueleza kuwa atapokea tuzo nyingi

sana mwaka huu na hizo tuzo ni ishara tosha ya


kudumu kwenye game kwa miaka kama hiyo ya

tuzo zake kwa maana ya miaka saba mbele yote

nyota yake itaendelea kung'ara" Alisema Dokta

Kamdege.

 

Aidha Mganga huyo aliendelea kusema" Unajuwa

haya mambo ya maagano yapo muziki na miti

shamba zinaendana kwani kwenye dunia hii ya

leo maadui ni wengi kuliko marafiki kwani wapo

watakaokuchukia bila sababu za msingi hivyo ni

vyema ukalijua mapema hilo na kujikinga kama

ilivyo kwa Diamond" Alisema mganga huyo

mwenyeji wa Mkoa wa Tabora.

 

Hata hivyo mganga huyo aliendelea kutoa uwito

kwa watanzania popote walipo duniani

waendelee kupata huduma zake kwani hii ni

kama baraka kwa taifa la Tanzania.

 

Dokta Kamdege amekuwa akitumiwa sana na

vigogo wa Serikali, wasanii na watu mbalimbali

duniani kufanikisha mambo yao kwa kuwapatia

baraka kupitia miti shamba.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger