skip to main |
skip to sidebar
PEMBE NA SENGA WAFUNIKA, NA KUSABABISHA MTAA KUFUNGWA KWA MUDA DAKIKA 45
WASANII nyota wa vichekesho Bongo, Ulimboka Mwalulesa ‘Senga
Kijumule’ na swahiba wake, Yusuph Kaimu Machoti ‘Pembe’ hivi karibuni
walifunga mtaa mjini Kahama baada ya mashabiki kuwazunguka kwa dakika 45
wakiwashangaa.
Wasanii nyota wa vichekesho Bongo, Ulimboka Mwalulesa ‘Senga Kijumule’(kulia) na swahiba wake, Yusuph Kaimu Machoti ‘Pembe’.
Wawili hao ambao walijipatia umaarufu mkubwa wakati walipokuwa
wakiigiza kupitia televisheni, walikuwa katika Wilaya za Mbogwe na
Kahama wakati wa uzinduzi wa albamu ya tatu ya msanii wa muziki wa asili
wa Kabila la Wasukuma aitwaye Bhudagala.
Wasanii hao wakiwa kazini.
Baada ya wananchi kuwaona wasanii hao wakitembea kwa miguu katika
mitaa mjini hapa, walianza kuwafuata taratibu na hatimaye kujikuta
wakiwa kundi kubwa ambalo halikutarajiwa.
No comments:
Post a Comment