WASANII WA MAREKANI WAUNGANA, SOMA SABABU YA WAO KUUNGANA HAPA

Picha ya mke wa Rais wa Marekani, Michelle Obama aliyotupia Twitter.
 
Hii ilitupiwa na Chris Brown kupitia Instagram.
....Msanii Waje kutoka Nigeria aliachia hii katika Instagram.
MASTAA kutoka kona mbalimbali za dunia wameungana katika kampeni ya #BringBackOurGirls inayoshinikiza kuachiwa kwa wasichana takribani 200 wa shule nchini Nigeria waliotekwa na wapiganaji wa Kundi la Boko Haram.
Kampeni hiyo inaendeshwa kupitia mitandao ya kijamii ambapo mastaa kama Chris Brown, Mary J Blige, 2Face, Keri, Waje na Mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama wameonekana kutupia picha zao wakiwa na mabango ya kampeni hiyo.
Kampeni hiyo inaendelea ikiwa ni wiki tatu zimepita tangu wasichana hao kutekwa nyara na Boko Haram.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger