MOYO unauma! Baada ya kutukanwa matusi ya nguoni kwenye mitandao ya
kijamii na blogs, kwa mara ya kwanza staa wa sinema za Kibongo,
Jacqueline Wolper Massawe amefunguka na kudai kwamba amechoka kutukanwa
kila kukicha lakini pamoja na hayo yote hatingishiki kwa lolote.
Habari zilieleza kuwa kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram,
Wolper amekuwa akitukanwa kila kukicha huku tetesi zikizagaa mtaani
kwamba mwanadada huyo ni msagaji. Matusi hayo yalikwenda mbele zaidi na
kudai kuwa kutokana na tabia yake ya usagaji ndiyo maana hataki kumweka
hadharani mwanaume wake.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita, Wolper alisema
kuwa ni kweli amechoka lakini anawaachia nafasi watu wanaomchafua kwenye
mitandao na hatishiki kwa lolote kwani maneno yao siyo ya kweli na
kamwe hatamtangaza mpenzi wake kama ilivyokuwa zamani.
“Watukane sana, waseme mimi ni mwanaume lakini mimi ninatambua
ninachokifanya, wakichoka wataacha. Kamwe sipo tayari kumweka mwanaume
wangu kwenye vyombo vya habari, unajua kwenye mitandao kuna uchonganishi
mwingi sana na mtu usipokuwa makini utajikuta ukimchukia mtu bila
sababu kutokana na watu kuwa na mitazamo mbalimbali,” alisema Wolper.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment