Benoit
Assou-Ekotto (kulia) akimsogelea mwenzake Benjamin Moukandjo baada ya
kipigo cha 4-0 kutoka kwa Croatia usiku wa kuamkia leo.
Benoit Assou-Ekotto akimtwanga 'ndoo' Moukandjo.
Samuel Eto'o akimtuliza Ekotto aliyepandisha hasira baada ya kichapo cha 4-0.
BEKI wa Cameroon, Benoit Assou-Ekotto aliamua kumpiga kichwa 'ndoo'
mchezaji mwenzake Benjamin Moukandjo kufuatia kipigo cha mabao 4-0 dhidi
ya Croatia.Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo wakati wa mechi ya Kombe la Dunia 2014 kati ya Cameroon na Croatia.
Katika mpambano huo Cameroon waliambulia kichapo cha mabao 4-0 na kuyaaga mashindano hayo baada ya kupoteza pia mechi yao ya kwanza dhidi ya Mexico kwa bao 1-0.
No comments:
Post a Comment