HISPANIA YAFUNGISHWA VIRAGO KOMBE LA DUNIA KWA AIBU


Iker Casillas na Iniesta wakitoka uwanjani vichwa chini baada ya kipigo.
Kocha wa Hispania, Vicente Del Bosque akiwa haamini kilichotokea.
Mchezaji wa Chile, Eduardo Vargas akiifungia timu yake bao la kwanza dakika ya 19.
Charles Aranguiz akifunga bao la pili kwa Chile.
KIKOSI cha mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia, Hispania kimeaga michuano hiyo baada ya kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Chile.
Mabingwa hao wa 2010 walipoteza mechi yao ya kwanza dhidi ya Uholanzi baada ya kulala kwa bao 5-1 kabla ya jana kupigwa tena na Chile.
Kwa matokeo ya jana, Hispania wanashikilia mkia katika kundi B wakiwa hawana pointi yoyote wakitofautiana mabao ya kufungwa na wenzao Australia ambao nao hawana pointi. Timu hizo zisizo na pointi zitakutana katika mechi yao ya mwisho Juni 23 mwaka huu.
Kundi hilo linaongozwa na Uholanzi wenye pointi 6 baada ya kushinda mechi zote mbili walizocheza.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger