skip to main |
skip to sidebar
CHAZ BABA AFUNGUKA NA KUSMA SAJENT AMEGOMEA MWANANGU
PREZIDAA wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ amefunguka
kuwa anatamani kuishi na mwanaye aliyezaa na mwigizaji Husna Idd
‘Sajent’ lakini mzazi mwenziye huyo amekuwa akimgomea.
Prezidaa wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ akiwa kwenye ofisi za Global Publishers.
Akizungumza na paparazi wetu, Chaz Baba alisema kabla hajaoa alikuwa
akimg’ang’ania akae naye lakini alipooa, amegeuka na kukataa katakata.
“Kiukweli simuelewi kabisa Sajent maana katika hali na akili ya
kawaida tu, sijaona mantiki ya kumkatalia mtoto wangu labda angeniambia
kama mwanangu amekataa mwenyewe hapo kidogo nisingekuwa na swali,”
alisema Chaz Baba.
Mwigizaji wa tasnia ya filamu Bongo, Husna Idd ‘Sajent’ aliyezaa na Chaz.
Chaz Baba ambaye alikuwa akibanjuka na Sajent miaka ya nyuma, kwa
sasa ni mume halali wa ndoa na bi dada anayefahamika kwa jina la Rehema.
No comments:
Post a Comment