MUIGIZAJI
wa sinema za Kibongo, Michael Sangu ‘Mike’ amejiuzulu ujumbe wa Bodi ya
Shirikisho la Filamu (TAFF) na kujiunga rasmi na Klabu ya Bongo Movie.
Akizungumza na paparazi wetu, Mike alisema amefikiri kwa kina na
kuona bora ajiengue katika Taff na badala yake aelekeze nguvu zake
katika Klabu ya Bongo Movie ambayo anaamini kwa sasa ni sahihi kwake.
“Nimeamua mwenyewe, sijalazimishwa na mtu, kila mtu na maamuzi yake,
acha kwa sasa niwe Bongo Movie kwani kila kitu kinakwenda na wakati,”
alisema Mike.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment