Miss
Tanzania 2001 na mwanamitindo wa kimataifa Millen Magese amekumbuka
kauli ya kwamba mipango si matumizi, kutokana na kuwa na
mipango mingi na marehemu Steven Kanumba enzi za uhai wake
katika kuikomboa sanaa ya filamu nchini Tanzania, lakini kabla
hawajakutana naye mauti yalimkuta...
Millen
na muigizaji maarufu nchini Nigeria, Ramsey Noah walipanga
kukutana na Kanumba lakini kabla siku hiyo haijafika kifo
kilimkuta Kanumba na mipango yote ikaharibika....
Millen |
Millen
alifafanua hayo katika mahojiano maalumu wakati akitangaza
kampeni yake ya kuhamasisha wanawake wanaosumbuliwa na maumivu
ya tumbo yasiyo ya kawaida pindi wanapokuwa katika mzunguko wa
hedhi zao ambapo kitaalam hujulikana kama Endometriosis ambapo
amegundua kwamba kati ya wanawake 100 wa Tanzania, wanawake 12
hadi 15 wanasumbuliwa na tatizo hilo...
Star wa Nigeria Ramsey Nouh na marehemu Steven Kanumba |
Akikumbuka
siku ya kifo cha Kanumba kabla hawajakutana na kuzungumzia
masuala mbalimbali kuhusiana na filamu za Tanzania na namna ya
kupiga hatua nyingine mbele,Millen alisema:
"Iliniuma
sana kipindi kile maana nilikuwa nipo nchini na tulipanga
mimi, Kanumba na Ramsey Noah lakini ndio ikawa hivyo lakini kwa
filamu zetu bado tunatakiwa kusoma zaidi ili tujue mambo
mengi na pia tutengeneze wigo mpana wa marafiki kutoka nje
kama mimi kwa sasa nina marafiki wengi akiwemo Ramsey Noah,
Genevieve Nnaji, Albal na wengine wa Marekani"
Katika
kusaidia tasnia hiyo, mrembo huyo anayemhusudu mrembo na
mwanamitindo Tausi Likokola,Iman,Flaviana Matata, na Harieth Paul
alisema mwelekeo wake baada ya kukamilisha masomo yake ya
uigizaji, ataandaa filamu yake binafsi itakayoelezea maisha yake
halisi na tatizo linalomkabili na pia ataandika hadithi
kuhusiana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, Albino.
"Kwa
sasa nasomea namna ya kuongoza filamu katika chuo cha New
York Film Academy nchini Marekani, nikimaliza nitaingia kwenye
filamu na kuleta mabadiliko katika uandishi wa hadithi za
filamu hizo tofauti na filamu nyingi za hapa nchini ambazo
nyingi hutambua zinavyoishia baada ya kuitazama mwanzo hivyo
kupoteza ladha ya kuitazama," alisema Millen na kuongeza:
Millen |
"Movies
zetu za hapa Tanzania zinakosa watunzi wazuri wa hadithi
maana nyingi zikianza unajua zitakapoishia,hivyo tunatakiwa
tujuane na wasanii mbalimbali kutoka nchi mbalimbali kama
ninavyowafahamu baadhi yao kutoka nchini Nigeria na baadhi ya
wasanii wakubwa nchini Marekani ndipo filamu zetu zitafika
mbali," anasema Millen.
Pia
model huyo wa kimataifa chini ya Ford Models New York alifafanua
sababu inayomfanya asishuke katika tasnia ya urembo akidai
inatokana na kujituma kwake, kujifunza zaidi na kutoridhika na
mafanikio aliyoyapata huku akiongeza kwamba anaishi na
kuwaheshimu vizuri wanaomuongoza pamoja na watu wote
wanaomzunguka hasa nchi yake.
No comments:
Post a Comment