Mambo hadharani! Uhusiano wa staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth
Michael ‘Lulu’ na mshiriki wa Shindano la Big Brother Africa 2013, Amir
Nando umewekwa kweupe.
Kabla ya wawili hao kufunguka, kulikuwa na madai mazito kuwa Lulu na
Nando ‘wanachepuka’ mara tu baada ya Nando kutolewa BBA kwa ukosefu wa
nidhamu.
Kuna habari kuwa Nando ndiye aliyevujisha ishu hiyo, jambo ambalo Lulu hakupendezwa nalo hivyo kumpiga chini.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, gazeti hili lilimtafuta Nando ambaye
mwanzoni alifanya kama utani akidai Lulu ni mwanamke anayefaa kuolewa
(wife material) lakini alipoulizwa kwa msisitizo, alikana kuwa na
uhusiano na mrembo huyo.
“Lulu ni mkali, niko tayari kumuoa lakini sijamwambia, akikubali freshi
nitamuoa. Kwa sasa ni mshikaji wangu tu na napenda kazi zake. Huwa ni
mtu ambaye napenda kufuatilia ishu zake,” alisema Nando.
Kwa upande wake Lulu alishtuka na kudai kuwa aulizwe huyohuyo Nando na si yeye kwani haoni sababu ya yeye kuulizwa.
Kwa upande wake Lulu alishtuka na kudai kuwa aulizwe huyohuyo Nando na si yeye kwani haoni sababu ya yeye kuulizwa.
Alifunguka: “Hebu muulizeni Nando kama ni Lulu mimi au mwingine? Yeye akishatoa jibu sina la kusema.”
No comments:
Post a Comment