HUU NDIO MSIMAMO WA KIONGOZI BONGO MUVI JUU YA MASHOGA NDANI YA CLUB HIYO

MWENYEKITI wa Klabu ya Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ (PICHANI JUU) amekataa katakata kuwataja wanachama wanaodaiwa ni mashoga ndani ya klabu hiyo ya jijini Dar.
Pichani ni baadhi ya wasanii wa Bongo Muvi.
Akizungumza na Amani juzikati jijini Dar baada ya kuombwa kuwataja wadaiwa hao, Steve alisema hashindwi kuyaanika majina yao, bali uongozi wake kwenye chama hicho si kuingilia mambo binafsi bali kuunganisha umoja na mshikamano kwa ajili ya tasnia ya filamu za Bongo.“Hilo suala kila mtu ananiachia mimi nilizungumzie kwa kukanusha au kuweka majina hadharani ya wanaodaiwa ni mashoga. Hadi namaliza uongozi wangu sitafanya hivyo,” alisema Steve.

Siku za hivi karibuni baadhi ya vyombo vya habari viliwahi kuripoti suala la kuwepo kwa mastaa mashoga kwenye klabu hiyo yenye nguvu ya ushawishi wa fedha mjini.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger