Supastaa wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’.
MSANII wa filamu anayefanya poa na muvi yake ya Zena
na Betina, Salma Jabu ‘Nisha’ amemnadi bwana’ake anayejulikana kwa jina
la Fahad baada ya kuweka picha kwenye ukurasa wake wa Facebook akiwa
amejichora ‘Mrs Fahad.’
Akizungumza na mwandishi wetu, Nisha alisema kuwa hawezi kuzungumza
chochote kuhusiana na mchoro huo kwa sasa lakini siku si nyingi ukweli
wote atauanika hadharani.
“Siwezi kuzungumzia chochote kuhusiana na hilo. Lakini hivi karibuni
nitamtambulisha rasmi na itakuwa ‘ofisho’ watu wangu wa Global msiwe na
wasi,” alisema Nisha.
No comments:
Post a Comment