Stori: issa mnally via GPL
UBABE! Tofauti na inavyoaminika na wengi
kuwa mfumaniwaji huwa mpole, kibao kimebadilika, mfanyakazi wa ndani
aliyejulikana kwa jina la Niachie amegeuka mbogo na kumchoma bisibisi
bosi wake, Amina ‘Mama Zai’ aliyemfumania akiwa na mumewe aitwaye Amri.
Tukio hilo lilitokea juzikati maeneo ya
Mbagala jijini Dar ambako mama Zai alimwekea mtego mfanyakazi wake huyo
wa ndani baada ya kubaini kuwa alikuwa akitembea na mumewe wakati yeye
akiwa kazini.
ISHU ILIVYOANZA
Akizungumza na paparazi wa kitengo
maalum cha kufichua maovu (OFM) siku mbili kabla ya tukio, mama Zai
alidai kuwa mumewe ana kawaida ya kufanya mapenzi na mfanyakazi wao wa
ndani wakati yeye akiwa kazini hivyo akaandaa mtego ili kukomesha tabia
hiyo.
KUMBE NI NESI
Mama Zai alizidi kumwaga data kuwa, yeye
ni nesi katika hospitali moja ya mtu binafsi iliyoko Jangwani jijini
Dar hivyo akiwa zamu ya usiku, mumewe hutumia mwanya huo kubanjuka na
hausigeli.
“Ananivizia nikitoka tu na akijua
nimeshafika mbali, anaingia chumbani kwa hausigeli na kuvunja naye amri
ya sita,” alidai mama huyo.
MTEGO WANASA
Mama huyo alisema ili kufanikisha zoezi
la kumnasa mumewe, alijifanya anakwenda zamu ya usiku kisha akajifungia
stoo ili aweze kufanya fumanizi matata.
Kama kawa, OFM ilitia timu nyumbani kwa
mama huyo ikiwa kamili na zana zake, ikakita kambi katika baa moja iliyo
jirani na nyumba hiyo na ilipofika saa tano usiku, ishu ikatiki, baba
Zai aliingia katika chumba cha mfanyakazi huyo kwa lengo la ‘kuharibu’.
'MISS IN ACTION’
Wakati makamanda wa OFM wakiwa
‘wanaseti’ kamera zao huku wakisubiri polisi na mwenyekiti wa serikali
za mtaa wafike eneo hilo, mama Zai alivamia chumba hicho (alihofia baba
atamaliza mchezo) na purukushani ya nguvu ikaanza.
Katika harakati za kujinasua katika
kipigo cha bosi wake, hausigeli huyo aliokota bisibisi na kumchoma mama
mwenye nyumba shingoni kisha kutimua mbio huku mume naye akiingia
mitini.
No comments:
Post a Comment