skip to main |
skip to sidebar
MAYA AFUNGUKA KUHUSU KIFO CHA RECHO
MSANII wa filamu Bongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’
amewataka wasanii wenzake kusameheana na kupendana kwani kifo cha msanii
mwenzao, Sheila Haule ‘Recho’ kimempa fundisho kubwa.
Baadhi
ya waombolezaji wakiwa katika hali ya huzuni katika mazishi ya marehemu
Recho Haule wengi wao wakiwa ni wasanii wa Bongo Muvi.
Akizungumza na paparazi wetu, Maya alisema vifo vya wasanii
vinavyotokea kila kukicha vinaumiza na kusikitisha hivyo wasanii
wanatakiwa kusameheana pale walipokoseana na kupendana kwani kifo kipo
wakati wowote.
Mayasa Mrisho,'Maya'(mwenye vazi la pinki) akiwa na msanii mwenzake wa Bongo Muvi, Shamsa Ford.
“Inahuzunisha hata mwezi haujapita tumeshawapoteza wasanii wawili
tunatakiwa kumuomba Mungu sana na wale wasanii wenye mabifu wapatane,
upendo utawale kati yetu kwani hatujui tunakufa lini,”alisema Maya.
No comments:
Post a Comment