Mbunge
wa Temeke, Abbas Mtemvu (kulia) akitazama hali ilivyobaki baada ya
bomoabomoa iliyofanywa na jiji kwenye vibanda vya mamalishe katika mtaa
wa Mbozi, Temeke.
Mmoja
wa Mamalishe eneo la Mtaa wa Viwanda la Mbozi, Temeke Dar es Salaam,
Amina Saidi (kushoto) akilalamika mbele ya Mbunge wa Temeke, Abbas
Mtemvu, mbunge huyo alipotembelea eneo la tukio kuona hali halisi jana.
Na Mwandishi Wetu
BOMOABOMOA ya vibanda vya mamalishe katika
eneo la Viwanda la Mbozi, Temeke Dar es Salaam, limezua mtafaruku
kufuatia mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu kuwakingia kifua
mamalishe hao.
Pamoja na kuahidi kuchukua hatua ya
kupambana kisheria na Halmashuri ya Jiji la Dar es Salaam, inayoendesha
bomoabomoa hiyo, Mtemvu amewata mamalishe kuendelea na shughuli zao
katika eneo hilo.
"Jambo hili la kunyanyasa wananchi kwa kuwafukuza katika maeneo bila kufuata taratibu halikubaliki hata kidogo.
Sasa mimi nawasaka watu hawa wa halmashauri
ili kuzungumza nao, lakini wakati nafanya hivyo nawaagiza mwendelee na
shughuli zenu hapa, na atakayekuja kuwafukuza mwambieni achukue kila
kitu nami nitapambana naye kisheria", Mtemvu amesema hayo jana wakati
akizungumza na baadhi ya mamalishe hao katoka eneo la viwanda la Mbozi.
Mtemvu alisema, Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Said Meck Sadick na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji
hawakupaswa kuwafukuza mamalishe hao kwa kutumia mgambo kuvunjavunja
vifaa na kuondoka na baadhi ya vyakula kama ambavyo imedaiwa, kwa sababu
ujenzi wa barabara waliyopo hautarajiwi kufanywa hivi karibuni.
Amesema mbali na ujenzi wa barabara hiyo
ambao Mtemvu alisema fedha za ujenzi amezitafuta yeye kama mbunge, pia
ilipaswa mamalishe hao kutengenezewa mazingira mengine ya kuendelea na
biashara zao kwa kuwa ni tengemeo kwa wafanyakazi kwenye viwanda
vinavyozunguka eneo hilo.
Mtemvu alisema kutimuliwa bila kufanyiwa
utaratibu mbadala, kutawafanya kinana mama, wasichana na vijana
wanaojishughulisha na biashara hiyo ya mamalishe sasa kutafuta njia
mbadala ya kuishi hata kama ni haramu jambo ambalo litakuwa siyo jema
kwa taifa.
Juzi, Jiji kwa kutumia mgambo na
tingatinga, walivamia eneo hilo la Mbozi na kusambaratisha vibanda vyote
vya mamalishe wasiopungua 35, na inadaiwa kwamba katika operesheni hiyo
mgambo
No comments:
Post a Comment